Dawa ya kuvimba mashavu ya uke,chanzo na Dalili zake
tatizo la kuvimba mashavu ya uke ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya Wanawake, je linatokana na nini? soma hapa zaidi..!!!!
TATIZO LA UKE KUWA MWEMBAMBA,KUKAUKA NA KUVIMBA(vaginal atrophy)
kuvimba kwa kuta za uke au kuvimba ukeni kwa kitaalam Vaginal atrophy,
Vaginal atrophy hili ni tatizo ambalo huhusisha uke wa mwanamke kuwa mwembamba,kukauka pamoja na kuvimba,(-)
Wanawake wengi hupata hili tatizo baada ya kufikia kipindi cha ukomo wa hedhi yaani Menopause
au wakati wa Ujauzito,mjamzito kuvimba uke
Shida hii ya shavu la uke kuvimba huweza kutokea kwenye shavu la Upande mmoja au sehemu zote mbili
Je tatizo hili la kuvimba uke chanzo chake ni nini?
CHANZO CHA TATIZO HILI au sababu ya kuvimba mashavu ya uke
sababu ya uke kuvimba au chanzo cha kuvimba mashavu ya uke ni nini?
Zipo sababu mbali mbali za kuvimba ukeni ikiwa ni pamoja na;
• Tatizo la Uwepo wa kiwango kidogo cha ESTROGEN mwilini kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
– Baada ya mwanamke kufikia ukomo wa hedhi
– Baada ya upasuaji wa kuondoa Ovary zote mbili
– Baada ya matumizi ya dawa ambazo huathiri uzalishaji wa kichocheo cha Estrogen kama baadhi ya dawa za kupanga uzazi
– Baada ya kupata huduma ya mionzi kwa ajili ya matibabu ya kansa hasa Pelvic Radiation
– Huduma ya Chemotherapy
N.k
• kuvimba uke kwa mjamzito au kuvimba uke wakati wa ujauzito
kuvimba uke kwa mama mjamzito ni hali ambayo huweza kutokea kwa baadhi ya wakina mama wajawazito, na chanzo kikubwa ikiwa ni mabadiliko ya vichocheo mwilini kwenye kipindi hiki.
Tatizo hili la kuvimba kwa mashavu ya uke huweza kuambatana na madhara mengine kama vile;
• Mwanamke kuwa mkavu ukeni
• Kuhisi hali ya kuungua ukeni
• Kutokwa na uchafu ukeni
• Kuwashwa sehemu za siri
• Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa
• Kukojoa mara kwa mara
• Kupata maambukizi ya ugonjwa wa UTI ambayo hujirudia rudia mara kwa mara
• Mwanamke kushindwa kuzuia mkojo kutoka yaani Urinary Incotinence
• Kutokwa na damu kidogo yaani Light bleeding wakati wa kufanya tendo la ndoa
• Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
• N.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA kuvimba kwa uke
Yapo matibabu mbali mbali kulingana na hali ya mgonjwa ikiwemo tiba ya uke kuwa mkavu,tiba ya ugonjwa wa kuvimba mashavu ya uke
Tiba mbali mbali za uke kuvimba ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa ya uke kuvimba n.k
– Zipo njia mbali mbali za kutibu tatizo hili kama vile; Matumizi ya dawa za kuongeza kiwango cha ESTROGEN mwilini mfano;
✓ Vaginal Estrogen Suppositories
✓ Vaginal Estrogen Cream
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!