Dawa ya Kuzuia KUKOROMA Usiku ukiwa Umelala

 Dawa ya Kuzuia KUKOROMA Usiku ukiwa Umelala/Usingizini,Pamoja na Chanzo

Baadhi ya watu hupatwa sana na tatizo hili la Kukoroma wakiwa wamelala mpaka kufikia hatua ya kujichukia,

Je chanzo cha Hali hii ni nini? Soma zaidi hapa..!!!

SABABU ZA KUKOROMA USINGIZINI

Hali hii hutokea pale ambapo kuna sababu au kitu chochote ambacho kimesababisha hewa isipite vizuri ukiwa umelala,

Ndipo kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni mtu kukoroma,

Kuna baadhi ya sababu mbali mbali huweza kusababisha mtu kukoroma akiwa usingizi,na baadhi ya sababu hizo ni kama vile;

- Kuwa mnene kupita kawaida,au mtu mwenye uzito mkubwa sana

- Kuziba kwa tundu za pua hali ambayo husababisha mtu kutumia nguvu sana kwenye kuvuta na kutoa hewa

- Wengine huanza kukoroma kutokana na allergic reaction za muda fulani,au wakiwa na tatizo la Sinus

- Kuwa na tatizo la nyama puani

- Misuli pamoja na nyama za koo na ulimi kulegea au kuwa dhaifu sana,

hali ambayo hupelekea kuanguka kwa nyuma sehemu ambapo hewa inapita

- Pia baadhi ya watu hurithi vinasaba vya tatizo hili kwenye familia

- Mtu kulala fofo au usingizi mzito sana

- Mtu kuchoka sana wakati wa kulala

- Unene

- Matumizi ya Pombe na Sigara ambapo huweza kupelekea kulegea kwa misuli ya koo

- Matumizi ya baadhi ya dawa kama dawa za usingizi n.k

- Mtu kulala vibayaa

- Kula vyakula vingi na vigumu sana wakati wa kulala N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!