DAWA YA MAFUA KWA WATOTO WADOGO
Moja ya vitu ambavyo huwasumbua sana watoto wadogo ni pamoja na mafua,kuharisha,kutapika,maumivu ya tumbo na homa.
Na ndyo maana kuna chanjo kabsa inajulikana kama ROTAX kwa lengo la kumzuia mtoto na shida ya kuharisha.
Mtoto mwenye shida ya mafua huweza kuambatana na shida zingine mfano;
• Mtoto kupiga chafya sana au kwa kitaalam hujulikana kama Sneezing
• Mtoto kukohoa mara kwa mara
• Macho ya mtoto kuwa mekundu kuliko kawaida
• Mtoto kukosa kabsa hamu ya kunyonya au kula chochote
• Mtoto kulia sana mara kwa mara
• Mtoto kukosa kabsa usingizi na kuhangaika tu muda wote
• Na wakati mwingine mtoto kuwa na homa au joto la mwili kuwa juu
Je mtoto mwenye mafua anasaidiwaje?
MATIBABU YA MAFUA KWA MTOTO MDOGO,
Kwanza kabsa,kabla ya kwenda kwenye matibabu unashauriwa kupambana na kuzuia vitu vyote ambavyo huweza kuwa chanzo cha mafua kwa mtoto wako kama vile;
- Kuzuia mtoto kukaa sehemu zenye vumbi sana
- Kuwasha Feni muda wote kwa watoto
- Kutumia mafuta au perfumes zenye harufu kali sana
- Kukaa na mtoto sehemu ambazo kuna shughuli zozote ambavyo huhusisha vumbi,uchanganyaji wa kemikali,dawa n.k
- Kukaa na mtoto mdogo sehemu ambavyo kuna moshi sana
- Mtoto kuchezea maji au kuwa katika hali ya unyevu unyevu muda wote ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo ambazo hazijakauka vizuri. n.k
TIBA AU DAWA YA MAFUA KWA WATOTO WADOGO
Kwa upande wa Tiba, Baada ya wataalam wa afya kumchunguza mtoto,huweza kumpatia dawa mbali mbali kama vile Sodium chloride nasal drops n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!