FAHAMU KWA KINA KUHUSU KIPIMO CHA CT SCAN
CT Scan ni kifupi cha maneno "Computed tomography" ambapo ni kifaa kinachotumia mfululizo wa X-rays pamoja na muunganiko wa Computers ili kugundua magonjwa mbali mbali,kuumia au majeraha mwilini kwa kupiga picha inayojulikana kama 3D image ya soft Tissues pamoja na Mifupa mwilini,
Kifaa hiki au kipimo hiki hakihusishi kusababisha maumivu ya aina yoyote kwenye mwili wako wakati wa utendaji kazi wake, hivo wataalam wa afya hukitumia sana ili kuona ndani ya mwili wako kuna tatizo la aina gani.
Wakati wa upimaji kwa Kutumia CT Scan,mgonjwa atalala chali kwenye (meza)kitanda cha mashine na ndipo taratibu kitanda kitaanza kusogea kuingia ndani ya mashine na kupata picha ya vipimo vinavyohitajika,na baada ya picha ya 3D kutoka kitanda cha mgonjwa hurudi chenyewe kuelekea nje.
JE UPIMAJI WA CT SCAN HUCHUKUA MUDA GANI?
Inategemea na muda wa maandalizi kwa mgonjwa kabla ya kuingia kwenye kipimo cha CT Scan pamoja na maandalizi ya kipimo chenyewe,hivo mchakato mzima huweza kuchukua dakika chache,nusu saa au hata saa moja,ingawa mchakato wa mashine yenyewe kufanya kazi huchukua muda mfupi sana kati ya dakika 10 mpaka 30, muda mwingi huweza kutumika wakati wa maandalizi.
KIPIMO CHA CT SCAN NI KWA AJILI YA KUPIMA NINI?
CT scan hutumika kuchunguza mifupa,viungo mbali mbali ndani ya mwili kama utumbo n.k,soft tissues,mishipa ya damu pamoja na uvimbe wowote unaokuwa,hivo baadhi ya kazi za CT Scan ni kusaidia;
1. Kugundua uvimbe(tumors),baadhi ya Saratani au Kansa kwa mgonjwa
2. Kugundua mifupa iliyovunjika(broken bones)
3. Magonjwa mbali mbali ya moyo
4. Tatizo la damu kuganda au kutengeza Clots
5. Matatizo mbali mbali kwenye utumbo,kama vile utumbo kuziba,magonjwa kama Crohn's disease n.k
6. Kuumia kwenye ubongo au Uti wa mgongo pamoja na magonjwa yanayohusisha ubongo au uti wa mgongo
7. Tatizo lolote linalohusisha damu kuvuja ndani ya mwili yaani Internal bleeding n.k
8. Pia Kipimo cha CT Scan hutoa majibu mazuri zaidi kuliko X-ray yenyewe hasa katika kuona vizuri viungo vya ndani ya mwili(organs) au Tissues na kusaidia wataalam wa afya kuona kila kitu kuliko kwenye X-ray N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!