Fahamu Kwa Kina Kuhusu Kipimo Cha Dna Au Vinasaba

 FAHAMU KWA KINA KUHUSU KIPIMO CHA DNA AU VINASABA PAMOJA NA GARAMA ZAKE(DNA-TEST)

Kipimo cha DNA au VINASABA yaani DNA-TEST ni kipimo ambacho watu wengi hukitaja sana kwenye jamii zetu hasa pale kunapotokea migogoro ya mahusiano na ndoa hata kuwa na mashaka kuhusu uhalali wa watoto waliopo au wanaotarajiwa kuzaliwa.

Je DNA Test ni nini?

DNA-TEST: Hiki ni kipimo ambacho hutumika ili kuweza kutambua mtoto aliyepo au anayetarajiwa kuzaliwa baba yake halali ni yupi?

Kipimo hiki hutoa majibu sahihi kwa asilimia 99.9% Hivo hutumika sana endapo kuna tatizo kutokana na sababu mbali mbali kwenye jamii,

Je kwanini kipimo cha DNA au VINASABA kitumike?

WATU HUTUMIA KIPIMO HIKI CHA DNA AU VINASABA KWA SABABU MBALI MBALI KAMA VILE;

- Ili kugundua uhalali wa Baba kwa mtoto fulani ambao huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;

• Migogoro ndani ya ndoa au mahusiano

• Mwanaume binafsi kutaka kujua matunzo na huduma anazotoa anatoa kwa mtoto wake kweli au ni kwa mtoto wa mwanaume mwingine?

• Swala la kiusalama wa Baba na mtoto pia

• Swala la kiuchunguzi zaidi mahakamani kutokana na Cases mbali mbali N.k

JINSI YA KUPIMWA KIPIMO CHA VINASABA AU DNA TEST

Zipo njia kuu mbili za upimaji wa kipimo cha VINASABA au DNA TEST, na Njia hizo ni (i) Kupitia njia ya kuchukua SAMPLE ya Damu yaani BLOOD-TEST (ii) Pamoja na Kutumia njia ya SWABS yaani CHEEK-SWABS

KUMBUKA: Kipimo hiki cha vinasaba au DNA kinaweza kufanyika baada ya Mtoto kuzaliwa au hata mama akiwa mjamzito,soma hapa chini

KIPIMO CHA VINASABA(DNA-TEST) KWA MAMA MJAMZITO

Baba wa mtoto huweza kujulikana hata kabla ya mtoto kuzaliwa, yaani mama akiwa mjamzito hasa katika ile miezi mitatu(3) ya kwanza ya ujauzito yaani First Trimester, na hapa kuna upimaji ambao huhusisha njia kuu TATU ambazo ni;

1. NONINVASIVE PRENATAL PATERNITY TEST(NIPP): kipimo hiki hufanya uchambuzi wa kina kuhusu DNA za mtoto ambaye yupo tumboni kwa mama ake hasa katika miezi mitatu ya kwanza yaani First Trimester, Hapa wataalam wa maabara huanza kulinganisha taarifa kutoka kwa DNA za mtoto na zile ambazo wamezitoa kwa Baba kutumia njia kama ile ya Cheek Swabs.

2. CHORIONIC VILLUS SAMPLING (CVS):Hapa wataalam wa afya au maabara huchukua Sample ya TISSUE kutoka kwenye Kondo la nyuma yaani PLACENTA kwa mama ambaye kabeba ujauzito huo,Kisha kuanza kulinganisha taarifa za DNA kutoka kwenye Sample hiyo na DNA au VINASABA kutoka kwa Mama na Baba, Njia hii ni hatari sana kwani huweza kusababisha tatizo la Mimba au Ujauzito kutoka.

3. AMNIOCENTESIS: njia hii huhusisha  wataalam kutoa kiwango kidogo cha maji ya uzazi yaani Amniotic Fluid kisha kuanza kuchukua taarifa na kuanza kulinganisha na taarifa za DNA kutoka kwa Mama na Baba.

GARAMA ZA KIPIMO CHA VINASABA AU DNA-TEST, JE KIPIMO HIKI HUGARIMU SHINGAPI?

swali hii watu wengi hujiuliza sana na wengine huanza kupewa majibu ambayo hayatoki kwenye vyanzo sahihi vya Taarifa hizo, Soma hapa Nukuu hii:

“Gharama ya kipimo cha vinasaba (DNA) ni Shilingi Laki moja kwa mtu mmoja, kwa hiyo kama wanaohitaji kupimwa ni Baba na Mtoto au Mama na Mtoto gharama ni shilingi Laki mbili” - Fideus Bugoye, Mratibu Kazidata ya Taifa ya Vinasaba vya Binadamu.

KUMBUKA: afyaclass haitoi huduma hii ya Upimaji wa Vinasaba au DNA-TEST,ila huu ni uchambuzi tu wa kukusaidia angalau kupata Mwanga juu ya Kipimo hiki cha DNA-TEST,

AU KAMA UNA TATIZO LINGINE LA KIAFYA UNAHITAJI USHAURI ZAIDI AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA ZETU:+255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!