Fahamu Kwa Kina Kuhusu Mashine Ya Mri

 FAHAMU KWA KINA KUHUSU MASHINE YA MRI

Bila shaka neno MRI sio geni kwako na kwa namna moja au nyingine umewahi kusikia mtu akisema mgonjwa kaambiwa afanyiwe kipimo cha MRI, japo unaweza usielewe hicho kipimo cha MRI ni nini na kinafanya kazi gani,karibu hapa ujifunze na upate kuelewa kuhusu kipimo cha MRI.

MRI-kirefu chake ni Magnetic resonance imaging, yaani ni aina ya mashine ambayo hutumia Sumaku kuscan au kupiga picha mwili wako kisha kutoa majibu wapi kuna tatizo, kipimo hiki huweza kuchunguza karibia kila sehemu kwenye mwili wako na kugundua tatizo lipo wapi, na sehemu hizo ni kama vile;

• Maeneo ya kichwani ikiwemo pamoja na Ubongo mzima

• Maeneo ya kwenye uti wa mgongo

• Maeneo ya kwenye mifupa pamoja na joints zote

• Maeneo ya moyo pamoja na Mishipa ya damu

• Maeneo ya kwenye matiti

• Viungo vya ndani kama vile Ini,Tumbo la uzazi yaani womb/uterus, tezi la Prostate n.k

JINSI MGONJWA ANAVYOPIMWA KWENYE KIPIMO CHA MRI

Mgonjwa hulala chali kwenye kitanda cha mashine ya MRI huku akiwa katanguliza kichwa au miguu kulingana na kitu gani kinatakiwa kuchunguzwa kwanza kisha kitanda chenyewe husogea na kumpitisha mgonjwa kwenye mashine kwa ajili ya kuchunguzwa maeneo mbali mbali ya mwili wake,

Zoezi hili huweza kuchukua muda wa dakika 15 na kuendelea kulingana na ukubwa wa tatizo na idadi ya picha ambazo huhitajika kuchukuliwa kutoka kwa mgonjwa.

JINSI KIPIMO CHA MRI KINAVYOFANYA KAZI

Mwili wa binadamu umetengenezwa kwa kiasi kikubwa cha Molecules za maji ambazo hujumuisha atoms za hydrogen pamoja na Oxygen, Katikati ya kila atom moja ya hydrogen kuna particle ndogo ambazo huitwa proton. Hizi Protons ni kama visumaku vidogo sana, hivo hupokea hisia kwa haraka sana baada ya kupitishwa kwenye mashine yenye sumaku kama MRI,

Na wataalam husema wakati umelala kwenye mashine ya MRI zile protons hujipanga kwenye mstari mmoja kama vile sumaku ikivuta sindano au kitu chochote chenye asili ya chuma, hivo kitendo hiki husababisha kutengenezwa kwa mawimbi yaani radio waves ambayo hutumwa moja kwa moja kwenye maeneo mbali mbali kwenye mwili wako kisha kukutana na protons ambazo zimejipanga kwenye direction moja,

Na hapa ndipo taarifa kuhusu maeneo mbali mbali ya mwili wako hutumwa na kupokelewa na kifaa ambacho kipo kwenye mashine ya MRI kinachojulikana kama RECEIVER, taarifa hizo husaidia kujua maeneo sahihi ambapo protons kwenye mwili wako zipo,kusaidia kutofautisha aina mbali mbali za tissue kwenye mwili wako, pamoja na kutoa taarifa kuhusu wapi kuna tatizo kwenye mwili wako.

JE MASHINE YA MRI NI SALAMA?

Kipimo hiki ni salama na wala hakisababishi maumivu yoyote kwenye mwili wako, japo kwa mgonjwa mwenye matatizo kama Caustrophobia anaweza asijisikie comfortable,

Tafiti mbali mbali zinaendelea kufanyika duniani kote kuhusu usalama wa mashine ya MRI na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kuhusu madhara ya mashine ya MRI,japo kipimo cha MRI hakiruhusiwi kufanyika kwa baadhi ya makundi ya watu kama vile;

- Wagonjwa waliowekewa kifaa cha PACEMAKER

- Wagonjwa waliowekewa joints za bandia yaani artificial joint

- Na pia kipimo cha MRI hakiruhusiwi kwa mama mjamzito

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!