Faida za kutumia kitanzi,Loop au copper IUD kama njia ya Uzazi wa Mpango

 Faida za kutumia kitanzi,Loop au copper IUD kama njia ya Uzazi wa Mpango,

Kwa Ulimwengu wa Sasa hivi swala la kupanga uzazi ni muhimu katika familia,

Na zipo njia nyingi ambazo watu hutumia ili kupanga uzazi, kama vile: kutumia kijiti,sindano,vidonge vya uzazi,kalenda, n.k

hapa tunazungumzia baadhi ya faida za njia hii ya Kitanzi au jina lingine Lupu ambayo huhusisha matumizi ya Copper Intrauterine device(IUD),

Njia hii imekuwa maarufu na kutumiwa na watu wengi Duniani kote,Na kutokana na takwimu za National Center for Health Research;

inakadiriwa kuwa zaidi ya watu million 100 hutumia njia hii duniani kote.

IUDs ni kifaa kidogo chenye umbo la T( T-shaped devices ) kama kwenye picha hapo, ambapo huwekwa kupitia ukeni na kuzuia mimba kutunga kwenye kizazi,

Intrauterine divice(IUDs) hizi zipo za aina mbali mbali ikiwemo:

- Hormonal IUDs: ambazo zina vichocheo ndani yake,hivi hutoa vichocheo au hormones aina ya progesterone kuzuia ujauzito

- Pamoja na copper IUDs: ambapo hivi havina vichocheo vyovyote ndani yake, badala yake kifaa kimezungushiwa copper wire,

Hii copper husababisha kinga ya Mwili kwenye kizazi kutoa majibu(immune response) ambayo yatafanya kuwa vigumu sana kwa mbegu za kiume kuishi ndani ya kizazi hivo kuzuia Ujauzito.

Hivo copper hii hutengeneza mazingira ya kuuma mbegu za kiume yaani toxic environment to sperm.

FAIDA ZA KUTUMIA AINA HII YA COPPER IUDs KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO

1. Uwezo wake wa kufanya kazi ni mkubwa, ikilinganishwa na njia nyingine za kupanga uzazi,njia hii hufanya kazi kwa zaidi ya asilimia 99%,

• mfano: Sindano au Depo-Provera shot: 94% effective.

• Vidonge(Pills), patches and vaginal rings: 91% effective.

• Condoms: 85% effective. n.k

2. Njia hii haina vichocheo vya aina yoyote(Non-hormonal ),

kwa sababu njia hii haina vichocheo vyovyote ndani yake,basi inafaa zaidi kwa wanawake wengi hasa kwa wanawake:

wanaoshi na tatizo la Saratani ya matiti,wanawake ambao wametumia njia za uzazi wa mpango zenye vichocheo ndani yake zikawaletea madhara makubwa, wanawake wenye tatizo la hormone imbalance n.k

3. Njia hii huweza kuzuia ujauzito kwa muda mrefu zaidi(Long-lasting),

Copper IUD huweza kuzuia ujauzito kwa Miaka 10 au wakati mwingine hadi miaka 12.

4. Kuanza kufanya kazi mapema, baada ya kuwekewa copper IUD huanza kufanya kazi mara moja au ndani ya muda mfupi sana

5. Uwezo wako wa kubeba MIMBA hurudi mapema sana pale unapohitaji kubeba mimba,

Hivo pale unapohitaji kubeba mimba unaongea na Daktari wako anatoa,na unaweza kubeba mimba ndani ya muda mfupi sana

tofauti na njia nyingine za uzazi kama vile Sindano; ambazo huweza kusababisha mwanamke kukaa kwa muda mrefu sana bila kubeba mimba hata baada ya kuacha kutumia.

6. Na wakati mwingine huweza kutumika kama njia ya dharura kuzuia mimba(emergency contraception),

endapo Copper IUD imewekwa ndani ya Siku 5 baada ya kufanya mapenzi bila kinga, huweza kuzuia wewe kubeba Mimba.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!