Ticker

6/recent/ticker-posts

Faida Za Tohara Kwa Mwanaume-afyatips(Mwanaume Kutahiriwa)



 FAIDA ZA TOHARA KWA MWANAUME-AFYATIPS(Mwanaume kutahiriwa)

Baadhi ya jamii bado hazijafahamu faida za wanaume kufanyiwa tohara na hasara kubwa ambazo huweza kutokea kwa wanaume ambao hawajafanyiwa tohara. katika makala hii tumechambua faida za mwanaume kufanyiwa tohara kama ifuatavyo;

FAIDA KWA MWANAUME MWENYEWE BAADA YA KUFANYIWA TOHARA NI PAMOJA NA;

- Mwanaume aliyetahiriwa huwa rahisi zaidi kujisafisha na kuondoa uchafu wote kwenye ngozi ya uume wake

- Mwanaume kutahiriwa hupunguza sana maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani Urinary tract infection(UTI)

- Mwanaume kutahiriwa hupunguza sana maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa yaani Sexual transmitted diseases(STD's)

- Mwanaume kutahiriwa hupunguza matatizo mbali mbali kwenye uume kama vile tatizo la phimosis ambalo huweza kusababisha ngozi ya mbele ya uume(foreskin) au kichwa cha uume kuvimba

- Mwanaume aliyetahiriwa huweza kufanya tendo la ndoa vizuri zaidi kuliko mwanaume ambaye hajatahiriwa

- Mwanaume kutahiriwa hupunguza tatizo la kansa ya uume yaani penile cancer n.k

FAIDA KWA MWANAMKE AMBAYE YUPO KIMAHUSIANO NA MWANAUME AMBAYE AMEFANYIWA TOHARA

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa huridhika kwa urahisi zaidi kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa,

Hii ni kwa sababu mwanaume aliyetahiriwa uume wake huweza kusimama kwa muda mrefu zaidi na kuwa na hamasa ya kurudia tendo mara nyingi zaidi kuliko mwanaume ambaye hajatahiriwa

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa huwa katika hatari ndogo zaidi ya kushambuliwa na magonjwa mbali mbali ya zinaa(STD's) kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa,

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba; Maambukizi ya kirusi cha Human papilloma virus(HPV),genital herpes,kaswende(syphillis), Trichomoniasis pamoja na maambukizi ya HIV hupungua zaidi endapo tendo la ndoa linafanyika na mwanaume akiwa ametahiriwa kuliko ambaye bado hajatahiriwa.

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa yupo kwenye hatari ndogo ya kupatwa na saratani ya mlango wa kizazi(cervical cancer) kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa,

• Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hajatahiriwa yupo kwenye hatari ya kuingiziwa uchafu kutoka kwa mwanaume,kushambuliwa na vimelea vya magonjwa kama vile bacterial vaginosis,yeast infection, pamoja na kushindwa kubalance kiwango cha PH ukeni, kuliko mwanamke ambaye hushirki tendo la ndoa na mwanaume ambaye katahiriwa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments