Ticker

6/recent/ticker-posts

Faida Za Unga Wa Ubuyu Na Mafuta Ya Mzeituni(Lishe Tips)



 FAIDA ZA UNGA WA UBUYU NA MAFUTA YA MZEITUNI(LISHE TIPS)

Katika makala hii tumechambua kuhusu Lishe, na leo tunazungumzia kuhusu faida za unga wa ubuyu pamoja na faida za mafuta ya mzeituni,huenda vitu hivi unavisikia tu au unavyitumia katika maisha yako ya kila siku lakini hujui faida zake. soma hapa chini..!!

FAIDA ZA UNGA WA UBUYU MWILINI NI ZIPI?

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.

Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwango cha Potasiamu kilichomo kwenye unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa watu wenye matatizo ya figo.

Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili (antioxidant) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi, bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha.

Hizo ndyo baadhi ya Faida za unga wa Ubuyu kwenye mwili wako,

FAIDA ZA MAFUTA YA MZEITUNI MWILINI NI ZIPI?

Mafuta ya mzeituni kama yakitumika vizuri yanaweza kuleta matokeo makubwa sana kwenye afya yako na kukusaidia kwa changamoto hizi;

Kutibu kisukari cha ukubwani (type 2 diabetes); Tafiti zinasema kwamba mafuta ya olive yakitumika kwa muda mrefu husaidia kupunguza athari ya kisukari na kuimarisha afya ya mgonjwa.

Kuimarisha afya ya moyo; kwa kurekebisha shinikizo la damu, kupunguza mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu (LDL) na pia kupunguza hatari ya damu kuganda kwenye mshipa ya damu.

Kupunguza hatari ya kupata saratani: Ukitumia mara kwa mara mafuta ya mzeituni unapunguza hatari ya kuugua saratani ya matiti na pia kiambata cha oleic acid kilichopo kwenye mafuta haya husadia kupambana na saratani.

Kupunguza hatari ya kupata ugonjwa unaoshambulia ubongo (Alzheimer’s disease)

Hizo ni baadhi tu, pitia post za nyuma nimeelezea zaidi

Je Utajuaje Mafuta yako ya Mzeituni ni feki!

Katika uchaguzi wa mafuta ya olive ni muhimu sana kuwa makini kwani mafuta mengi yanayouzwa ni feki na yamejaa kemikali hatari kwa afya yako. kama mafuta yako ni feki utaona harufu hizi;

Harufu ya karanga zilizoharibika na ladha kama ya grisi

Harufu ya kuchacha au harufu ya uvundo kama sox zilizovaliwa

Harufu ya vumbi au fangasi

Harufu ya vinegar/siki N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments