Ticker

6/recent/ticker-posts

Hamasisha mwananchi yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Macho kwenda Hospitali



TUHAMASISHANE KWENDA HOPITALI KWA WENYE DALILI ZA TRAKOMA

Na WAF - Dar Es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ametoa rai kwa Watanzania hasa wa Mkoa wa Pwani kushirikiana na Serikali kumhamasisha mwananchi yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Macho kwenda Hospitali kwakuwa ugonjwa huo husababisha upofu. 

Waziri Mhagama amesema hayo leo Septemba 18, 2024 wakati wakiwa katika ziara pamoja na Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) ambae ni Mke wa Mtoto wa Mfalme wa Uingereza walipotembelea Kituo Cha Afya cha Mlandizi Mkoa wa Pwani kwa lengo la kujionea utoaji huduma za matibabu ya macho

“Yapo magonjwa ambayo hayajapewa kipaumbele sio Tanzania tu bali Duniani kote ikiwemo ugonjwa huu wa macho ( Trakoma) lakini pia magonjwa kama mabusha , matende, minyoo ya tumbo, kichocho.” Amesema Waziri Mhagama 

Waziri Mhagama amshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya Uingereza kwa kuamua kufanya kazi ya kutokomeza magonjwa haya amabyo hayapewi kipaumbele. 

Kwa upande wake, Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) ambae ni Mke wa Mtoto wa Mfalme wa Uingereza amesema lengo lao ni kuhakikisha Tanzania inatokomeza magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.

“Haya yote yanawezekana kupitia ushirikiano ambao tunautoa kwa Tanzania ikiwa ni kwa mtu mmoja mmoja katika kutokomeza magonjwa ya Trakoma.” Amesema Bi. Sophie

Amesema, Kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uingereza, kwa pamoja wanaweza kutokomeza ugonjwa huo wa Trakoma kutokana na uzoefu wa magonjwa mengine waliyoweza kuyatokomeza.

Ziara hiyo imemalizika kwa kumtembelea  nyumbani kwake mnufaika wa matibabu ya Ugonjwa wa  Trakoma yanayotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau akiwemo Sightsavers.



VIKOPE

• • • • •

UGONJWA WA VIKOPE(TRAKOMA),CHANZO,DALILI NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa wa Vikope ambapo kwa kitaalam hujulikana kama TRAKOMA,ni ugonjwa ambao hutokea kwenye Kope za macho na kusababisha kope kujikunja kwa ndani hivo kuleta msuguano kati ya kope na kiyoo cha mbele cha jicho.

CHANZO CHA UGONJWA WA VIKOPE(TRAKOMA)

Ugonjwa wa Vikope au Trakoma husababishwa na Bacteria Jamii ya Klamidia Trakomati. Ambapo baada ya mgonjwa kushambuliwa na bacteria hawa matokeo yake ni kujikunja kwa kope kwa ndani nahivo kuleta hali ya msuguano mkubwa ndani ya jicho.

Madhara ya Ugonjwa wa trakoma

MADHARA YAKE;

- Mgonjwa kupata maumivu makali ndani ya jicho kwa sababu ya msuguano

- Jicho kubalika rangi na kuwa jekundu

- Mgonjwa kupata tatizo la uharibifu wa sehemu ya nje ya jicho yaani KONEA

- Lakini pia Mgonjwa anaweza kuwa Kipofu kabsa.

DALILI ZA UGONJWA WA VIKOPE(TRAKOMA)

• Mgonjwa kuwashwa na jicho lilioathirika

• Jicho kutoa machozi lenyewe

• Jicho kutoka uchafu kama matongotongo

• Rangi ya jicho kubalika na kuwa nyekundu

• Mgonjwa kupata maumivu makali ya jicho

• Kuwa na hali ya Msuguano ndani ya jicho

• Kope kuvimba na kujikunja kwa ndani,hivo sehemu ya ndani kuonekana kwa Nje.

MATIBABU YA UGONJWA WA VIKOPE(TRAKOMA)

Matibabu ya Ugonjwa wa Trakoma au Vikope ni pamoja na Matumizi ya Dawa kama Azthromycin na Tetracycline. Lakini ni vizur kwenda hospital kuchunguzwa kwanza kabla ya kutumia Dawa yoyote.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments