Idadi ya vifo,mafuriko nchini Myanmar yaongezeka

Idadi ya vifo,mafuriko nchini Myanmar yaongezeka

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko makubwa nchini Myanmar kufuatia kimbunga Yagi imeongezeka maradufu hadi kufikia 226. Taarifa hii imeripotiwa na chombo cha habari cha serikali ya Myanmar.

Kimbunga Yagi kilipiga maeneo ya kaskazini mwa Vietnam, Laos, Thailand na Myanmar zaidi ya wiki moja iliyopita huku kikiandamana na upepo mkali na mvua kubwa na kusababisha mafuriko na maporomoko ya tope ambayo yamesababisha vifo zaidi ya 500 kwa mujibu wa takwimu rasmi.

 Wakala wa kushughulikia majanga wa Afisi ya Umoja wa Mataifa ya utatibu wa misaada ya kibinadamu UNOCHA, umesema watu wanaokadiriwa kufikia 631,000 wameathiriwa na mafuriko kote nchini Myanmar.

UNOCHA imesema chakula, maji ya kunywa na nguo vinahitajika kwa dharura na imetahadharisha kwamba barabara zilizofungwa na madaraja yaliyohabiriwa yanakwamisha kwa kiwango kikubwa juhudi za utoaji wa misaada. 

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!