Ticker

6/recent/ticker-posts

Je Ni Kweli Kwamba Kula Limao Na Ndimu Kunakausha Damu Au Hupunguza Damu?



 JE NI KWELI KWAMBA KULA LIMAO NA NDIMU KUNAKAUSHA DAMU AU HUPUNGUZA DAMU?

Hii ni dhana ambao watu wengi wanayo kwenye jamii zetu, lakini soma hapa chini kufahamu ukweli;

Matumizi ya Limao au Ndimu,Hii ni jamii ya matunda yenye wingi wa Vitamin C ambavyo husaidia sana kwenye Ufyonzwaji wa Madini ya Chuma au kwa Kitaalam hujulikana kama absorption

Na madini chuma ni muhimu sana kwenye utengenezaji wa chembe chembe nyekundu za damu na hivo kusaidia kuongeza damu,

Hivo basi kutokana na maelekezo hayo badala ya limao au ndimu kupunguza damu kama wengi wanavyofikiria, huweza kusaidia pia kwenye kuongeza damu mwilini.

SUMMARY:

1. Machungwa na Ndimu yana Wingi wa Vitamin C

2. Vitamin C husaidia sana kwenye ufyonzwaji wa madini ya Chuma yaani kwa kitaalam absorption,

Hivo wingi wa Vitamin C ndyo ufyonzwaji mzuri na uwepo wa madini ya chuma kwa kiwango kikubwa zaidi Mwilini

3. Madini ya chuma,ni muhimu sana mwilini kwani husaidia utengenezwaji wa chembechembe nyekundu za damu,

au kwa maana nyingine rahisi madini ya chuma husaidia kuongeza damu

4. Hivo Matunda jamii ya Limao na Ndimu husaidia kuongeza damu na sio kupunguza damu kama watu wengi wanavyofikiria

ZIJUE FAIDA ZA KULA CHUNGWA NA CHENZA(TANGARINE) KATIKA MWILI WAKO

Tunda la Chungwa limekuwa likipatikana katika Maeneo mengi sana,hungu wengine wakila tu bila hata Kujua umuhimu wake Mwilini.

Kumbuka chakula na Matunda ni Tiba katika Mwili wako.

Hizi hapa ni baadhi ya Faida za Tunda la Chungwa pamoja na Chenza

Faida za Chungwa na Chenza ni Pamoja na;

1. Chungwa na Chenza ni vyanzo vizuri vya VITAMIN C

2. Husaidia Kuboresha Mfumo mzima wa KINGA ya MWILI
3. Husaidia kuzuia Uharibifu wa NGOZI
 
4. Huboresha Presha Ya Damu
 
5. Hushusha Kiwango cha Cholesterol Mbaya
6. Husaidia kudhibiti kiwango cha Sukari Mwilini
 
7. Hupunguza Hatari ya Kupata Tatizo la Saratani au Kansa
 
8. Husaidia Kuboresha afya ya Macho

9. Husaidia kuzuia tatizo la kupata Choo kigumu
N.K.....!!

JE WEWE UNA DESTURI YA KULA MACHUNGWA NA MACHENZA?

Kama huna utaratibu huu,anza leo kwani tunda hili ni muhimu sana katika afya yako.Kumbuka afya yako Kwanza..

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!!



Post a Comment

0 Comments