Jinsi ya kutambua pete feki za dhahabu, kwa wale wanaotarajia kufunga Ndoa
Jinsi ya kutambua pete feki za dhahabu, kwa wale wanaotarajia kufunga Ndoa
Wapenzi wengi kabla ya kufunga ndoa wamekuwa na utamaduni wa kutumia pete yenye mwonekano wa madini ya dhahabu wakiamini au kuaminishwa kuwa imetengenezwa kwa madini halisi ya dhahabu.
Hata hivyo, Ofisa wa Madini kutoka maabara ya Tume ya Madini Tanzania (TMC), Edith Lewis amesema siyo kweli kila pete yenye rangi ya dhahabu ina dhahabu.
Edith amesema wananchi wengi wanatapeliwa kwa rangi ya dhahabu wanapokusudia kununua vito vya madini ya dhahabu.
“Ukichukua madini ya shaba na zinki ukachanganya inaleta mng’ao wa dhahabu kama unavyoweza kuiona dhahabu, lakini pia kuna madini ya Nikeli, Tungsten na titanium hutumika kwenye mchanganyiko wa kupata mng’ao wa dhahabu,”amesema Edith.
Edith ametoa kauli hiyo leo Oktoba 26, 2023 wakati wa kufunga kongamano hilo jijini Dar es Salaam, akidai kupokea wateja mbalimbali walioshtushwa na matokeo ya vito vyao baada ya kuhakiki.
Katika band hilo, tume hiyo inaendelea kutoa huduma mbalimbali za ushauri, utoaji wa taarifa na usaidizi wa masuala ya madini na upimaji wa vito vya thamani kw akutumia maabara yake.
“Tumepokea zaidi ya 10 leo na wengi ni akina mama, wanakuja kupima pete, heleni na mikufu, baadhi wanashangaa kuona tofauti na thamani halisi ya vito vyao au kuona madini tofauti,”amesema.
“Kwa hiyo tunashauri kujenga utamaduni wa kuhakiki kwenye maabara za madini.”
Miongoni mwa waliohakiki ni pamoja na Dk Jackson Makubi aliyenunua Sh2 milioni miaka saba iliyopita. Matokeo ya vipimo yalibaini pete yake ina uzito wa gramu nne pamoja na mchanganyiko wa dhahabu kwa asilimia 87.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!