Ticker

6/recent/ticker-posts

Kahawa huweza Kupandisha Presha(shinikizo la Damu)



 Kahawa huweza Kupandisha Presha(shinikizo la Damu)

Hushauriwi kutumia kahawa kama tayari una tatizo la Presha ya kupanda,

mbali na kwamba baadhi ya watu hutumia kahawa kwa lengo la kupoteza Usingizi,lakini kahawa pia inaweza kupandisha presha yako ndani ya muda mfupi baada ya kutumia.

Machapisho zaidi ya 34 ya tafiti mbali mbali yanaonyesha kwamba;

200–300 mg za caffeine kutoka kwenye Kahawa sawa na makadirio ya kikombe kimoja na Nusu(1.5) mpaka vikombe viwili(2) vya kahawa,

huweza kuongeza presha kwa kiwango cha 8 mm Hg na 6 mm Hg kweny systolic na diastolic blood pressure,

Na mabadiliko hayo yalionekana ndani ya masaa 3 tu baada ya mtu kutumia Kahawa,

Ongezeko hilo hutokea kwa watu wote,walio na presha ya kawaida(normal bp), walio kwenye hatari ya kupata presha, na ambao tayari wanashida ya presha.

Lakini pia kwa kadri mtu anavyozoea kutumia Kahawa mara kwa mara hutengeneza kitu kinaitwa caffeine tolerance mwilini,

Ndo mana matokeo ya kahawa kwa siku za mwanzo,ni tofauti kadri unavyotumia mara kwa mara, hata kwenye swala la presha ni hivo hivo.



Post a Comment

0 Comments