Kimbunga Yagi chawasili Vietnam baada ya kuipiga China

Kimbunga Yagi chawasili Vietnam baada ya kuipiga China

Kimbunga Yagi ambacho ndiyo kikubwa zaidi kurikodiwa kwa mwaka huu barani Asia, kimewasili kaskazini mwa Vietnam leo baada ya kulipiga eneo la kusini mwa China jana na kusababisha maafa ikiwamo vifo vya watu wawili.

Kimbunga hicho kilianzia nchini Ufilipino mapema wiki hii na kusababisha vifo vya watu 16 na hapo jana kiliwasili kwenye kisiwa cha China cha Hainan, na dhoruba yake iling´oa miti na kuharibu miundombinu ya nishati na barabara.

Mamlaka za Vietnam zimesema kilipowasili mapema leo asubuhi kwenye mji wa pwani wa Haiphong kilikuwa kinasafiri kwa kasi ya kilometa 160 kwa saa.

Sehemu ya mji huo ulio na idadi kubwa ya viwanda imeshuhudia uharibifu kidogo kwenye majengo na huduma ya umeme pia imetatizika.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!