Kubanwa Pumzi Na Kupumua Kwa Shida

 KUBANWA PUMZI NA KUPUMUA KWA SHIDA

Kuna wakati hali hii huweza kumtokea mtu kwa muda mfupi tu na kupotea hasa kwa baadhi ya watu wakiwa kwenye hali ya wasiwasi au hofu kubwa.

ila mara nyingi hili ni tatizo ambalo huweza kuhusisha matatizo mengine ikiwemo shida ya mapafu pamoja na moyo.

HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA KUBANWA PUMZI NA KUPUMUA KWA SHIDA

1. Mtu kuwa na ugonjwa wa Asthma

Ugonjwa huu husababisha njia za hewa kuvimba pamoja na kuwa nyembamba sana hali ambayo huathiri hewa kupita vizuri na kusababisha matatizo kama vile;

- mtu kukosa hewa na kupumua kwa shida(shortness of breath)

- Kupumua na kutoa hewa yenye sauti zisizo za kawaida yaani wheezing sound

- Mtu kubanwa sana na kifua

- Mtu kukohoa n.k

2. Ugonjwa wa Pneumonia

Ugonjwa huu huhusisha maambukizi kwenye mapafu ambayo husababisha kuvimba na kujaa maji pamoja na usaha kwenye vifuko vya hewa ndani ya mapafu,Kisha kuleta madhara kama vile;

- Mtu kubanwa na pumzi,kupumua kwa shida au kukosa hewa

- Mtu kuanza kukohoa pamoja na maumivu makali ya kifua

- Joto la mwili kuwa juu sana au mtu kuwa na homa kali

- Mwili kutetemeka sana na kutoa jasho sana

- Kupatwa na maumivu ya misuli n.k

3. Wakati mwingine maambukizi ya magonjwa kama CORONA, huweza kusababisha shida ya mtu kubanwa sana na mbavu,kukosa hewa,kushindwa kupumua n.k

4. Mtu kuanguka na kuumia kwenye mbavu,kifua au moyo huweza pia kuchangiq tatizo hili la kukosa pumzi na kushindwa kupumua.

5. Tatizo la Chronic obstructive pulmonary disease (COPD)

ambapo mgonjwa huweza kupatwa na shida mbali mbali kama vile;

- Kukosa pumzi,kupumua kwa shida au kukosa hewa

- Kupatwa na shida ya kikohozi ambacho ni endelevu

- Kifua kuwa kizito sana na kupata maumivu makali ya kifua n.k

6. Tatizo la Pulmonary embolism

Ambapo huhusisha kuziba kwa mishipa ya arteries ndani ya mapafu kutokana na damu kuganda au kutengeneza clots,

Hali hii ya damu kuganda au kutengeneza clots mwilini na kuanza kuziba kwenye vimishipa vya damu huweza kuleta madhara kama;

- Mtu kukosa pumzi au kushindwa kupumua

- Miguu kuanza kuvimba

- Kupata maumivu makali ya kifua

- Mtu kukohoa sana

- Kupatwa na tatizo la kizunguzungu kikali

- Mapigo ya moyo kubadilika kabsa

- mtu kupoteza fahamu

- Mwili kutoa jasho sana kuliko kawaida n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!