kuwashwa kwapani,chanzo chake ni nini?

kuwashwa kwapani,chanzo chake ni nini?

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha tatizo la kuwashwa kwapani, na katika makala hii tumekuchambulia baadhi ya sababu hizo;

1. Tatizo la Mzio(allergies),

Unaweza kuwa na shida ya Allergies kwa baadhi ya vitu ikiwemo; deodorant, shaving cream,Sabuni za kuogea,baadhi ya mafuta,Maji ya kuogea ambapo kitaalam hujulikana kama Aquagenic urticaria n.k.

Tatizo hili la Allergy huweza kusababisha shida ya kuwashwa kwapani.

2. Maambukizi ya Fangasi, Baada ya kushambuliwa na fangasi-Yeast infection (Candida), mtu huweza kuonyesha dalili mbali mbali ikiwemo;

  • Ngozi kubadlika rangi na kuwa nyekundu eneo lililoathiriwa
  • Kupatwa na miwasho kwapani
  • Kutoa harufu mbaya zaidi n.k.

Candida ni fangasi ambao hukua katika mazingira ya joto na unyevunyevu kama vile kwapani n.k.

Kuwa mzito kupita kiasi, kuwa na kisukari, au matumizi ya baadhi ya dawa za kuua vijasumu(antibiotics) kunaweza kukuweka katika hatari ya kupata maambukizi haya ya fangasi kwenye ngozi.

Zipo dawa mbali mbali za kutibu fangasi hawa(antifungal medications) ikiwemo;

  • Vidonge kama fluconazole
  • Au za kupaka kama clotrimazole au ketoconazole.

Kama una Ugonjwa wa Kisukari,hakikisha unaidhibiti sukari yako, kwani kwa kufanya hivo inasaidia kuzuia maambukizi ya fangasi kurudi tena.

3.  Kuwa na tatizo la Contact dermatitis, ambapo ngozi ya kwapani huwa katika hali ya kuungua,kuwaka moto,kuwasha n.k baada ya kugusana na baadhi ya vitu.

4. Tatizo la Folliculitis, ambapo vishungi vya nywele yaani hair follicle huvimba baada ya mashambulizi ya bacteria kama vile staphylococcus aureus.

Bacteria hawa huweza kupenya kwenye ngozi wazi kwapani wakati wa kunyoa nywele kwa kutumia wembe au ukiwa na kidonda kwapani n.k

Tatizo hili huweza kusababisha muwasho kwapani pamoja na maumivu.

5. Ingrown hairs, Unaweza kupata shida ya muwasho kwapani wakati nywele yenyewe inakua tena kwenye ngozi.

6. Kuwa na magonjwa kama vile Psoriasis,

Psoriasis ni tatizo ambalo huhusisha mfumo wa kinga mwili(autoimmune disorder), Hapa mwili wenyewe huanza kushambulia seli za ngozi ambazo hazina shida yoyote.

Hii inaweza kuleta dalili kama vile; Ngozi kuwa nyekundu, kuwa na magamba,kuwaka moto,miwasho sana n.k.

7. Mashambulizi ya fangasi ambao hupenya kwenye ngozi-Tinea corporis (ringworm) n.k

Kama unatatizo la kuwashwa kwapani hakikisha unapata matibabu mapema.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!