Maambukizi kwenye Sikio la mtoto,chanzo,dalili na Tiba

Maambukizi kwenye Sikio la mtoto,chanzo,dalili na Tiba

Maambukizi kwenye Sikio hutokea wakati Vimea vya magonjwa kama vile Virus au bacteria wanaposhambulia sehemu ya kati kwenye sikio(middle ear) ambapo kwa kitaalam maambukizi haya hujulikana kama Otitis media.

Mara nyingi maambukizi kwenye Sikio huambatana na maumivu ya sikio,uchafu kutoka n.k, na kwa baadhi ya watoto tatizo hili hupona lenyewe.

Kwanini Watoto hupata maambukizi kwenye Sikio kwa urahisi zaidi kuliko watu wazima?

Watoto hupata maambukizi ya sikio mara nyingi zaidi kuliko watu wazima kwa sababu:

1. Sehemu ya sikio inayojulikana kama eustachian tubes haifanyi kazi sawa na watu wazima, hali ambayo husababisha maji kukusanyika nyuma ya ngoma ya Sikio(eardrum).

2. Kinga yao ya mwili bado haina uwezo wa kupambana na vimelea vya magonjwa vyakutosha

3. Wana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa kutoka kwa watoto wengine.

Dalili za Maambukizi kwenye Sikio

Dalili za Maambukizi kwenye Sikio ni pamoja na;

  • Kupata maumivu ya Sikio
  • Kukosa hamu ya chakula
  • Kupata shida ya Usingizi
  • Kupata shida ya Kusikia au kutokusikia vizuri kwenye sikio lililoathiriwa
  • Kuhisi hali ya Uzito,pressure au kujaa ndani ya Sikio lako
  • Kutokwa na usaha au uchafu sikioni,uchafu ambao huweza kuwa na rangi ya njano,brown au nyeupe n.k

USHAURI: Usiweke chochote kwenye mfereji wa sikio ikiwa una uchafu au maji kutoka kwenye sikio lako, Kitu chochote kinachogusa ngoma ya sikio iliyopasuka kinaweza kusababisha uharibifu zaidi.

Chanzo cha Maambukizi kwenye Sikio

Bakteria na virusi husababisha maambukizi kwenye sikio. Mara nyingi, maambukizi ya sikio huanza baada ya baridi au maambukizi mengine ya njia ya juu ya kupumua. Vijidudu huingia kwenye sikio lako la kati kupitia bomba la eustachian (eustachian tube).

Mara tu Virusi au bakteria wanapoingia ndani ya sikio wanaweza kusababisha mrija wa eustachian kuvimba. kuvimba huku kunaweza kusababisha mrija kuziba, na hivyo kusababisha kutokufanya kazi vizuri na maji maji kwenye sikio lako la kati kupata maambukizi.

Vitu hivi huongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye sikio

• Umri: Watoto wachanga na watoto wadogo (kati ya miezi 6 na miaka 2) wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya sikio.

• Family history: Kupata maambukizi ya sikio kunaweza kuwa tatizo ndani ya familia yako

• Mafua: Kuwa na mafua huongeza hatari ya kupata maambukizi ya sikio. Watoto walio katika vituo vya kulelea watoto wachanga na katika vikundi wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa au kupata maambukizi kwenye masikio kwa sababu wana uwezekano mkubwa wa kuwa karibu na watoto walio na mafua au magonjwa mengine ya kupumua ambayo ni yakuambukiza.

• Magonjwa ya muda mrefu(Chronic illnesses): Magonjwa ya muda mrefu ikiwemo magonjwa ambayo husababisha upungufu wa kinga mwilini pamoja na magonjwa sugu ya kupumua (kama vile cystic fibrosis na pumu au Asthma), yanaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya sikio.

• Sababu zingine ambazo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya sikio ni pamoja na;

  • Uvutaji wa Sigara
  • Kuwa kwenye mazingira ya moshi
  • Uchafuzi wa hali ya hewa
  • Uchafu wa mwili n.k

Madhara ya Maambukizi ya Sikio kwa Mtoto

Madhara ya Maambukizi ya Sikio ni pamoja na;

- Kupoteza uwezo wa kusikia

- Mtoto kuchelewa kuongea, Fahamu ili mtoto ajifunze Lugha na kuendelea kuongea anahitaji kusikia, hivo endapo maambukizi ya sikio yataathiri uwezo wa mtoto kusikia, hata kuongea pia inaweza kuwa tatizo kwake.

- Kupasuka kwa ngoma ya Sikio,Takriban asilimia 5% hadi 10% ya watoto walio na maambukizi ya sikio hupasuka kidogo kwenye ngoma ya sikio. Mara nyingi, mpasuko huu hupona wenyewe. Ikiwa sivyo, mtoto wako anaweza kuhitaji upasuaji.

- kusambaza maambukizi zaidi, Maambukizi yasiyotibiwa au maambukizi yasiyopona yenyewe yanaweza kuenea.

Maambukizi haya yanaweza kuenea kwenye mfupa nyuma ya sikio lako (mastoiditis). Mara kwa mara, maambukizi yanaweza kuenea kwenye utando unaozunguka ubongo wako na uti wa mgongo (meninji) na kusababisha homa ya uti wa mgongo(meningitis).

Matibabu ya Maambukizi ya Sikio

Matibabu yanategemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na:

Umri wa mtoto wako.

Ukali wa maambukizi.

Asili ya maambukizi (maambukizi ya mara ya kwanza, yanayoendelea au ya kurudia).

Ikiwa maji yanabaki kwenye sikio la kati kwa muda mrefu.n.k

Mara nyingi, maambukizi ya sikio hupona bila matibabu. Mtoa huduma wako anaweza kufuatilia hali ya mtoto wako ili kuona kama inaimarika kabla ya kuagiza matibabu. Mtoto wako anaweza kuhitaji dawa za kuua vimelea vya magonjwa au upasuaji kwa maambukizi ambayo hayatoki. Wakati huo huo, dawa za maumivu zinaweza kusaidia kwenye dalili kama vile maumivu ya sikio.

Dawa za maumivu ambazo huweza kutumika ni pamoja na;

  • acetaminophen (Tylenol®)
  • ibuprofen (Advil®, Motrin®)

Kamwe Usimpe mtoto aspirini. Aspirini inaweza kusababisha hali ya kutishia maisha inayoitwa Reye’s syndrome.

Zingatia haya ili kuzuia maambukizi ya sikio kwa Mtoto

- Hakikisha unamkinga mtoto na magonjwa yanayoathiri mfumo wa hewa(respiratory illnesses) ikiwemo mafua.

- Epuka kabsa uvutaji wa Sigara au kukaa kwenye mazingira yenye moshi wa Sigara

- Hakikisha unamnyonyesha mtoto wako kwa kipindi cha miezi sita bila kumchanganyia na kitu chochote, bila kusahau kuendelea kunyonyesha hadi miaka 2 au zaidi hata baada ya kuanza kumpa na vitu vingine.

Maziwa ya mama hutoa kinga ya kutosha kwa mtoto,Antibodies kwenye maziwa ya mama hupambana na virusi na bakteria wanaosababisha maambukizi.

- Hakikisha mtoto anapata chanjo zote muhimu anazotakiwa kupewa. n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!