Madhara ya kula nyama ya ng'ombe mbichi

 


Madhara ya kula nyama ya ng'ombe mbichi

Ni desturi ya baadhi ya watu kula nyama mbichi, lakini je hii ni Salama kwa afya yako?

Kula nyama mbichi yoyote ikiwemo nyama mbichi ya ng'ombe unajiweka kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa,kwa kitaalam "foodborne illness"

Magonjwa haya husababishwa na kula nyama yenye vimelea vya magonjwa kama vile bacteria, Virusi, parasite na hata viambato vya sumu(toxins).

Hawa ni Vimelea ambao hupatikana zaidi kwenye nyamba mbichi;

  •  Salmonella,
  • Clostridium perfringens,
  • E. coli,
  • Listeria monocytogenes,
  • Campylobacter

Nyama ya ng'ombe mbichi huweza kubeba vimelea kama hawa kisha kusababisha magonjwa kwa binadamu baada ya kula nyama kama hiyo,

Lakini ukiwa umepika nyama yako vizuri viini vyote hivi vya magonjwa huharibiwa/kufa hata kabla ya kula na kuingia mwilini mwako.

Fahamu pia,Unaweza kupata Magonjwa kama vile BRUCELLA kwa kula nyama mbichi au nyama ambayo haijapikwa Vizuri kiasi cha viini vya magonjwa kufa.

Soma Zaidi hapa kuhusu ugonjwa wa BRUCELLA

Dalili ya Ugonjwa unaotokana na kula nyama ya ng'ombe mbichi(foodborne illness)

Ikiwa umekula nyama yoyote mbichi kisha viini vya magonjwa vikapata nafasi ya kuingia mwilini mwako huweza kusababisha ugonjwa "foodborne illness", na hizi ni baadhi ya dalili ambazo zinaweza kujitokeza kwako;

- Kuhisi kichefuchefu

- kutapika

- Kuharisha

- kuanza kupata maumivu makali ya tumbo

- Kupata Homa

- Pamoja na kupata maumivu ya Kichwa

Kwa kawaida, Dalili hizi hujitokeza ndani ya Saa 24, na huweza kudumu kwa muda wa siku 7 au Zaidi kulingana na baadhi ya kesi, viini husika vya ugonjwa n.k

Kwa ujumla, kupika vizuri nyama ya ng'ombe huharibu vijidudu vinavyoweza kuwa na madhara. Kwa upande mwingine, pathogens hubakia katika nyama mbichi. Kwa hivyo, kula nyama mbichi huongeza sana hatari ya kupata ugonjwa unaosababishwa na chakula, na unapaswa kuendelea kuchukua tahadhari.

Kundi lilipo kwenye hatari zaidi ya kuugua

Watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata Madhara yanayotokana na kula nyama mbichi ya ng'ombe ni pamoja na;

  • watoto,
  • wanawake wajawazito
  • au wanaonyonyesha,
  • Pamoja na watu wazima/wazee,

Watu hawa Wanapaswa kuepuka kula nyama mbichi kabisa.

Hitimisho

Ulaji wa nyama mbichi ya ng'ombe au nyama nyingine yoyote mbichi sio salama kabsa kwa afya yako, hakikisha unakula nyama ambayo imepikwa Vizuri.

Kula nyama mbichi yoyote ikiwemo nyama mbichi ya ng'ombe unajiweka kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa,kwa kitaalam "foodborne illness"

Magonjwa haya husababishwa na kula nyama yenye vimelea vya magonjwa kama vile bacteria, Virusi, parasite na hata viambato vya sumu(toxins).

Hawa ni Vimelea ambao hupatikana zaidi kwenye nyamba mbichi;

  •  Salmonella,
  • Clostridium perfringens,
  • E. coli,
  • Listeria monocytogenes,
  • Campylobacter

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!