Madhara ya Kutumia Flagyl Kuzuia Mimba: Hatari za Matumizi ya Dawa hii kwa Afya ya Wanawake
Wanawake wengi hupata changamoto za kiafya kuhusiana na uzazi, ikiwa ni pamoja na changamoto ya kuzuia mimba. Kutokana na sababu tofauti, wanawake wengi huchagua njia mbadala za kuzuia mimba. Moja ya njia hizi ni matumizi ya dawa kama vile Flagyl.
Flagyl ni dawa ambayo hutumika kutibu magonjwa mbalimbali, kama vile maambukizi ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi, tumbo na Utumbo. Hata hivyo, matumizi ya Flagyl kuzuia mimba yanaweza kuwa hatari kwa afya ya wanawake.
Duniani kote baadhi ya wanawake hutumia njia za hatari sana kuzuia Ujauzito, Flagyl ni dawa ambayo huweza kutumika kutibu magonjwa mbali mbali ikiwemo maambukizi yanayotokana na parasites yaani parasitic infections kama vile;
- Maambukizi ya Giardia kwenye utumbo mdogo(Giardia infections),
- Maambukizi ya Amoeba(amebic liver abscess,amebic dysentery n.k),
- Tatizo la bacterial vaginosis,
- trichomonas n.k
Flagyl sio dawa ambayo ipo kwenye Kundi la dawa za kuzuia Ujauzito na wala haina uwezo wa kuzuia Mimba kama Wanawake wengi wanavyoambiwa,
Na hata baada ya Kubeba Ujauzito, Matumizi ya dawa aina ya Flagyl hasa kwenye miezi 3 ya kwanza(first trimester) hukatazwa(Contraindicated) kwa Sababu huweza kuleta madhara kwa mtoto aliyetumboni.
Makala hii itajadili madhara ya kutumia Flagyl kuzuia mimba na jinsi ya kuepuka hatari za matumizi ya dawa hii kwa afya yako.
Madhara ya Kutumia Flagyl Kuzuia Mimba
1. Kuongeza Hatari ya Mimba kutunga Nje ya Mji wa Mimba(ectopic pregancy)
Kutumia Flagyl kuzuia mimba kunaweza kuongeza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi au nje ya mji wa mimba.
Hii ni hali hatari sana ambayo husababishwa na yai kutungwa nje ya mji wa mimba. Inaweza kusababisha maumivu makali, kuvuja damu na hatimaye kuhatarisha maisha ya mwanamke.
SOMA ZAIDI HAPA: Uhusiano kati ya matumizi ya Flagyl na mimba Kutunga Nje ya Kizazi
2. Kutokupata Mimba
Matumizi ya Flagyl kuzuia mimba yanaweza kusababisha tatizo la kushindwa kwa mwanamke kupata mimba pale anapohitaji kubeba ujauzito.
Hii ni kwa sababu dawa hii inaweza kuleta athari kwenye mfumo wa uzazi wa Mwanamke na kusababisha ugumba(Infertility).
3. Madhara mengine ya kiafya
Matumizi ya Flagyl kuzuia mimba yanaweza kusababisha madhara mengine ya kiafya kama vile:
- Maumivu ya tumbo
- Kutapika na kichefuchefu
- Maumivu ya kichwa
- Kupata Kizunguzungu
- Uchovu na hali ya kutojisikia vizuri
Jinsi ya Kuepuka Hatari za Matumizi ya Flagyl kuzuia Mimba
- Tumia Njia Salama za Kuzuia Mimba
Kutokana na hatari zinazohusiana na matumizi ya Flagyl kuzuia mimba,
ni vyema kutumia njia mbadala salama za kuzuia mimba kama vile mipira ya kondomu, vidonge vya kuzuia mimba na kadhalika.
- Tumia Dawa kwa Uangalifu
Ikiwa unapaswa kutumia Flagyl kwa matatizo mengine mbali mbali, hakikisha unapata maelezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya
- Muone Daktari au Wataalam wa afya Kwa Ujumla
Ni muhimu kuongea na wataalam wa afya kabla ya kuanza kutumia Flagyl kuzuia mimba,
Utapewa ushauri sahihi kuhusu dawa hii na jinsi ya kuepuka hatari zake. Pia utapewa njia mbadala za kuzuia mimba ili kuepuka hatari za matumizi ya Flagyl.
FAQs
[sc_fs_multi_faq headline-0="h3" question-0="Je, Flagyl ina athari kwa mimba?" answer-0="Matumizi ya Flagyl yanaweza kuathiri mimba na Kusababisha madhara kama vile mimba kutunga nje ya kizazi/mji wa mimba, kuharibu mfumo wa uzazi kwa mwanamke na kusababisha ugumba." image-0="" headline-1="h3" question-1="Je, ninaweza kupata mimba baada ya kutumia Flagyl?" answer-1="Inawezekana kupata mimba baada ya kutumia Flagyl lakini kuna hatari ya kuharibu mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba. Ni vyema kuongea na daktari wako kabla ya kuanza kutumia dawa hii ili kupata ushauri sahihi." image-1="" count="2" html="true" css_class=""]
Hitimisho
Matumizi ya Flagyl kuzuia mimba yanaweza kuwa hatari kwa afya ya wanawake,
Hii ni kwa sababu Flagyl Inaweza kusababisha madhara kama vile;
- Kuongeza hatari ya mimba Kutunga nje ya Kizazi/mji wa mimba(ectopic pregnancy),
- kuharibu mfumo wa uzazi kwa mwanamke,
- na kusababisha ugumba(Infertility).
Ni vyema kutumia njia mbadala salama za kuzuia mimba,Hivo zungumza na wataalam wa afya kabla ya kutumia Flagyl ili kupata ushauri sahihi,
Kuepuka matumizi mabaya ya dawa kama Flagyl kuzuia mimba ni muhimu kwa afya ya wanawake.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!