Madhara ya rangi za magari,Soma hapa Kufahamu
Kama ilivyozoeleka kwenye masikio ya watu, kila kitu kina faida zake pamoja na hasara zake.
Hata rangi ambazo tumezoea kuziona zikipendezesha vitu mbali mbali,zina faida zake na hasara zake.
Hapa tunazungumzia rangi ambazo hupakwa kwenye vitu mbali mbali kama vile; rangi za magari, rangi za kuta za nyumba,rangi za michoro na picha mbali mbali, N.K
Tafiti za afya zinaonyesha kwamba ndani ya rangi hizo kuna kemikali mbali mbali ambazo huweza kuleta madhara mbali mbali katika mwili wa binadamu kama vile Saratani, Magonjwa ya vifua,mapafu, N.K
Hizi hapa ni baadhi ya kansa au Saratani ambazo huweza kuchangiwa na uwepo wa kemikali hizo kwenye rangi mbali mbali;
– Saratani ya damu
– Saratani ya mapafu
– Saratani ya koo
– Saratani ya kongosho
– Saratani ya mdomo
– Saratani ya kibofu
– Saratani ya Ngozi
Madhara ya rangi za magari
Fahamu Rangi za Magari huwa na baadhi ya Kemikali ndani yake ambazo nyingine sio Nzuri kabsa kwa Afya yako,
Kemikali hizi zote zinaweza kusababisha madhara mbali mbali ikiwemo;
- kuvimba kwenye Njia ya hewa au Magonjwa kwenye mfumo wa Upumuaji,
- pamoja na upele wa ngozi na kuvimba Mwili,
- Kupata athari zinazotokana na allergies(mzio),
- uharibifu wa neva na ubongo,
- Kupata shida ya kichefuchefu,
- kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya Viungo,
- maumivu ya kichwa
- Pamoja na kutapika.
Wafanyakazi wa magari na rangi hushauriwa kutumia zana mbali mbali za kujikinga na kemikali hizi hatari kutoka kwenye Rangi.
Uchoraji wowote wa kutumia Rangi za Magari za kupulizia(Automobile spray painting) unachukuliwa kuwa kazi ya hatari kwa kuongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa yanayohusu mfumo wa Upumuaji kwa kitaalam "respiratory diseases".
Kwa ujumla, wachoraji wanaotumia Rangi za magari za Kupulizia wameonyesha kuwa na Uwezo mdogo wa Mapafu yao kufanya kazi(Lower Pulmonary function)
Vimumunyisho vyenye sumu (Toxic solvents) kwenye rangi za Magari huongeza hatari ya Kupata Tatizo la Kupoteza usikivu(Huathiri uwezo wa Masikio kusikia),
Wafanyakazi wa magari na rangi hushauriwa kutumia zana mbali mbali za kujikinga na kemikali hizi hatari kutoka kwenye Rangi.
Pia Utafiti ya NCBI ulionyesha; Tatizo hilo la kupoteza Usikivu kwenye Masikio lilihusishwa na mazingira ya kazi ambayo ni ya kelele.
Post:Hayo ndyo baadhi ya Madhara ya Rangi za Magari.
NB; Hivo basi, kwa wewe ambaye unafanya kazi zozote zinazohusu rangi, unashauriwa kujikinga sana kwa kuvaa nguo za kufunika mwili wako wote kama vile Evarol, Kofia ngumu kichwani, boot miguuni pamoja na mask usoni ili kujikinga na kuingiwa na rangi hizi kwenye mwili wako.
Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba,afya yako ndyo mtaji wako wa kwanza.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!