MADHARA YA TANGAWIZI KWA MJAMZITO
- Ukweli ni kwamba wakina mama wengi wajawazito hutumia tangawizi,hasa pale wakipatwa na shida kama vile kichefuchefu pamoja na kutapika,
hali ambazo huweza kuanza kwenye miezi 3 ya mwanzo kwenye ujauzito yaani First tremester
Hali ya kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito kwa kitaalam hujulikana kama Hyperemesis gravidarum na Emesis Gravidarum.
Endapo matumizi ya Tangawizi ni ya kiwango kidogo sana mfano Gram 1 ya Tangawizi Mbichi na sio ile ya Unga, sio tatizo kwa mama mjamzito.
• Pia Tangawizi hii huweza kutumiwa na Wajawazito ambao wapo kwenye hatari ya kupatwa na kisukari cha Mimba yaani Pre diabetic Gestational, na ni chanzo kizuri cha Calcium,madini chuma,Zinc n.k
MADHARA YA TANGAWIZI KWA MAMA MJAMZITO
- Endapo mama mjamzito utatumia tangawizi kwa kiwango kikubwa unaweza kupatwa na madhara mbali mbali kama vile;
1. Kuharibu mimba hasa ikiwa changa kama umetumia kwa kiwango kikubwa
2. Kupatwa na shida ya mvurugiko wa tumbo mara kwa mara
3. Kupatwa na shida ya kiungulia zaidi kwa baadhi ya wajawazito
4. Kupatwa na tatizo la maumivu makali ya kichwa kwa baadhi ya wajawazito
5. Na wengine huweza kupatwa na matatizo kama vile maumivu makali ya tumbo, kuharisha n.k
KUMBUKA; Endapo unatumia dawa kama Nifedipine,Metformin,Insulin,Asprin, Ongea kwanza na wataalam wa afya kabla ya matumizi ya Tangawizi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!