Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara Ya Ugonjwa Wa Pid,fahamu hapa



 MADHARA YA UGONJWA WA PID

 PID-Pelvic Inflammatory disease,huu ni ugonjwa ambao unahusu maambukizi ya Bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke. 

Tafiti zinaonyesha kwamba,kati ya wanawake nane(8) waliowahi kuugua PID basi mmoja wao atakuwa na shida ya kupata mimba hapo baadae, 

Huku wale waliopata ujauzito wakiwa kwenye hatari ya kupatwa na matatizo mbali mbali kama vile; -Mimba kuharibika zenyewe - Kujifungua kabla ya wakati - Na wengine kupatwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi yaani Ectopic pregnancy. 

MADHARA YA UGONJWA WA PID NI PAMOJA NA;

 • Mimba kutunga nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy, PID ambayo haijapata tiba huweza kusababisha kovu kwenye tissue yaani Scar tissues ndani ya mirija ya uzazi(fallopian tubes),

 Hii huweza kupelekea Scar tissues kuzuia yai lililorutubishwa kupita na kwenda kujishikiza kwenye mji wa mimba, matokeo yake mimba huendelea kukua kwenye mirija ya uzazi yaani Fallopian tubes nje ya kizazi.

 • Uwezo wa kubeba mimba kupotea yaani Infertility, PID huweza kuharibu via vya uzazi vya mwanamke, na kusababisha mwanamke kushindwa kushika mimba au kubeba mimba,

 Hivo unavyokuwa kwenye hatari ya kupata PID mara kwa mara au PID kutokutibiwa unakuwa kwenye hatari zaidi ya kupoteza uwezo wako wa kuzaa(infertility)

 • Kupata shida ya maumivu ya kiuno ambayo hayaishi(Chronic Pelvic pain), maumivu haya huweza kudumu kwa miezi au hata miaka bila kupona, 

Na hii hutokana na PID kusababisha Kovu(Scars) ndani ya mirija yako ya uzazi(fallopian tubes) pamoja viungo vingine, Na matokeo yake pia,ni maumivu makali sana wakati wa PERIOD(hedhi) au wakati yai linatoka kwenye Ovary yaani kipindi cha Ovulation. 

• Tatizo la Tubo-Ovarian abscess, PID huweza kusababisha hali ya usaha kujikusanya kama jipu kwenye njia ya uzazi hasa kwenye maeneo ya mirija ya uzazi(fallopian tubes) pamoja na vifuko vya mayai(ovaries), 

Na kama hali hii isipopata tiba huweza kuhatarisha maisha yako(Life-threatening Infection).

 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584. 





Post a Comment

0 Comments