Mambo ya kuzingatia kwenye utunzaji wa Kitovu cha Mtoto mchanga
Mambo ya kuzingatia kwenye utunzaji wa Kitovu cha Mtoto mchanga
MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE KITOVU CHA MTOTO BAADA YA KUZALIWA
Baada ya mama kujifungua kitovu cha mtoto hukatwa na kutenganisha mawasiliano kati yake na mtoto,hivo mtoto kujitegemea mwenyewe.
YAPO BAADHI YA MAMBO MUHIMU SANA YA KUZINGATIA KUHUSU KITOVU CHA MTOTO
1-Mama hakikisha kitovu cha mtoto hakivuji damu baada ya kukatwa na kufungwa na mtaalam wa afya.
2-Kitovu hudondoka chenyewe,ambapo kwa asilimia kubwa kwa watoto wengi ndani ya wiki moja,kitovu huwa tayari kimeshadondoka.
3-Hakikisha kitovu cha mtoto hakitoi usaha,au kubalika rangi hasa ya manjano na kutoa harufu mbaya,hii sio dalili nzuri.
4-Usiweke kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto mpka kidondoke chenyewe.
5-Epuka imani potofu kama zile za kuweka mavi ya Ng'ombe n.k,kwenye kitovu cha mtoto.
6-Ni muhimu kuhakikisha eneo hili la kitovu Cha mtoto linakuwa kavu muda wote.
Matumizi ya vitu kama spirit au chumvi kama wakina mama walivyokuwa wanashauriwa kuweka kwenye kitovu cha mtoto hapo zamani hayafai,
Kwani baadhi ya tafti zinaonyesha kuwa uwekaji wa spirit katika kitovu huuwa bacteria wazuri wanaosaidia kitovu kukauka kwa haraka na vizuri zaidi.
7-Hakikisha mtoto anavalishwa nguo ambayo haitamtonesha eneo la kitovu:
8-Pia unashauriwa kumfunga au kumvisha mtoto vizuri pampers ili isiguse eneo la kitovu Cha mtoto wala usikifunike na pampers.
KUMBUKA; JUKUMU LANGU KWAKO NI KUKUSHAURI,KUKUELMISHA NA KUKUPA MSAADA WA KIAFYA PALE INAPOHITAJIKA.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!