Matumizi ya SP kwa Mama Mjamzito(kinga dhidi ya Malaria)

Matumizi ya SP kwa Mama Mjamzito(kinga dhidi ya Malaria)

Kutokana na mabadiliko makubwa ambayo Mwanamke huyapata kipindi cha ujauzito,

Vitu vingi hubadilika ikiwemo mabadiliko kwenye mfumo mzima wa kinga ya mwili yaani body immune system hali ambayo hupelekea mwanamke mjamzito kushambuliwa na magonjwa kwa urahisi zaidi.

kushuka kwa kinga ya mwili kunakopelekea kushindwa kupambana na maambukizi ya Malaria,uwepo wa organ mpya kama vile Placenta(kondo la nyuma), pamoja na kuwepo kwa sehemu mpya ambazo Parasites wanaweza kujishikiza,

vyote hivi huweza kuchangia mama mjamzito kuugua Malaria kwa haraka zaidi.

MADHARA YA UGONJWA WA MALARIA KWA MAMA MJAMZITO

Madhara ya Ugonjwa wa Malaria kwa mama mjamzito ni makubwa zaidi,

Madhara haya huweza kuwapata wote,mama pamoja na mtoto aliyetumboni,

Baadhi ya Madhara hayo ni Pamoja na;

- Kusababisha tatizo la kuisha damu kwa mama mjamzito yaani maternal anemia,

hali ambayo huweza kuhatarisha maisha ya mama na mtoto aliyetumboni.

- Mtoto kufariki akiwa tumboni(fetal loss)

- Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake yaani premature delivery

- Kudhoofisha ukuaji wa mtoto aliyetumboni(intrauterine growth retardation)

- Kuzaa mtoto mwenye tatizo la Uzito mdogo sana n.k

Madhara yote haya huongeza hatari ya Mama pamoja na mtoto kupoteza maisha kabla na baada ya kujifungua.

MATUMIZI YA SP KWA MAMA MJAMZITO

Watu wengi hujiuliza,kwanini Mama mjamzito hana Malaria lakini anapewa Dawa za Malaria,

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba Dawa hizi za SP ambazo mama mjamzito hupewa kwenye mahudhurio ya Kliniki,

Sio kwa ajili ya kutibu Ugonjwa wa Malaria,ila ni kwa ajili ya kumkinga Mama mjamzito na ugonjwa wa Malaria yaani hutumika kama "intermittent preventive treatment of malaria"

Hivo hata kama huna Malaria ukiwa mjamzito, bado dawa hizi ni muhimu kwako.

Moja ya njia ya kumkinga mama mjamzito na ugonjwa wa malaria ni pamoja na Matumizi ya dawa hizi aina ya sulfadoxine-pyrimethamine au kwa kifupi SP, Kulala kwenye chandarua n.k

Hakikisha unajikinga na Malaria ili kuwa Salama Wewe Pamoja na Mtoto aliyetumboni.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!