Ticker

6/recent/ticker-posts

Maumivu Ya Chini Ya Kitovu,Mgongo Na Matiti Baada Ya Kujifungua/Kuzaa



MAUMIVU YA CHINI YA KITOVU,MGONGO NA MATITI BAADA YA KUJIFUNGUA/KUZAA

Maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu,
mgongo na matiti mara baada ya
kujifungua/kuzaa na ambayo huongezeka
wakati wa kunyonyesha kitaalamu yanaitwa "afterpains"

Mara kadhaa watu wamekuwa wakiamini kuwa maumivu yanayoambatana na zoezi zima la kujifungua hupotea mara baada ya kujifungua. Kitu ambacho inawezekana si sahihi kwa wote.

Nyakati za awali mara baada ya kujifungua inaaminika kunakuwa na mabafiliko katika baadhi ya maeneo ya ubongo ambayo kwa namna moja ama nyingine hupelekea fikira na mitazamo ambayo hupelekea kuhisi maumivu makali isivyo kawaida.

Kuzaa kwa upasuaji au kuzaa kwa njia ya kawaida lakini kwa kusaidiwa na vifaa kunaambatana na maumivu makali baada ya kujifungua ukilinganisha na unapozaa kawaida. Kwa kawaida maumivu haya hutegemea hisia, mawazo na mtazamo.

Maumivu ya tumbo hutokea ikiwa ni matokeo ya mji wa mimba kunywea au kupungua kwa mji wa mimba katika hatua ya kurudi katika umbo la awali kabla ya kubeba ujauzito.

Namba ya nzao inahusishwa na kiwango cha maumivu haya. Katika mimba ya kwanza maumivu haya huweza kuwa sio makali sana n uweza kuisha ndani ya muda mfupi, lakini baada ya mimba mbili na kuendelea inaaminika maumivu huongezeka kutokana ukweli kuwa misuli ya mji wa mimba inakuwa imepunguza nguvu ya mvutano hivyo hupitia katika kipindi cha kunywea na kujilegeza hivyo kupelekea maumivu kuwa endelevu kwa muda.

Mimba zenye mapacha, watoto wakubwa, kiwango kikubwa cha maji katika mfuko wa mtoto, maambukizi nk zinaaminika kuambatana na maumivu haya mara baada ya kujifungua.

Kunyonyesha huweza kuleta au kuongeza kiwango cha maumivu kwasababu kitendo cha kunyonyesha hupelekea kutolewa kwa homoni ya oxytocin ambayo huchochea kunywea kwa mji wa mimba na hivyo maumivu.

Maumivu haya huweza kuwa chini ya kitovu, mgongoni au kwenye matiti.

Asilimia 64 ya kinamama hufananisha maumivu haya na maumivu ya hedhi. Baadhi hufananisha na maumivu au hisia mtoto akicheza awapo tumboni, wengine hufananisha na maumivu ya njaa na wengine huyafananisha na kitu kigumu kinachotembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

NAMNA YA KUZIA AU KUPUNGUZA
kukojoa mara kwa mara, kulalia tumbo (kulala kifudi fudi) AU kujikanda na maji ya vuguvugu inaweza kusaidia.

Matumizi ya dawa , za kutuliza maumivu, hupelekea kukata au kutulia kwa maumivu haya

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments