Mgonjwa atolewa Ini badala ya bandama kisha kupoteza maisha
Serikali ya Jimbo la Florida huko Marekani imemfungia Leseni ya Udaktari na kuagiza kusimamishwa kazi Daktari aitwae Thomas Shaknovsky baada ya kutuhumiwa kutoa ini la Mgonjwa badala ya Bandama wakati wa upasuaji na kusababisha Mgonjwa huyo kuvuja Damu nyingi hadi kupelekea kifo chake.
Kupitia taarifa ya dharura iliyotolewa na Idara ya Afya ya Jimbo la Florida, imesema kuwa Dkt. Thomas Shaknovsky wa Hospitali ya Ascension Sacred Heart Emerald Coast iliyopo Miramar Beach, Florida aliondoa ini la Mkazi wa Alabama, Bill Bryan (70) badala ya bandama na kusababisha hatari kubwa kwa Mgonjwa huyo ambaye alifariki dunia baada ya upasuaji huo.
Imeelezwa kuwa Daktari huyo baada ya kutambua kosa lake alijaribu kuficha taarifa za upasuaji kwa kutengeneza rekodi za matibabu zenye kudanganya juu ya kile kilichotokea na kuwashinikiza Manesi waliokua wakimsaidia katika upasuaji huo kusema uwongo na sasa Familia ya Marehemu imefungulia kesi kwa kusababisha kifo kwa uzembe.
“Mume wangu alifariki akiwa hoi kwenye meza ya chumba cha upasuaji na Dkt. Shaknovsky, sitaki Mtu mwingine yeyote afe kutokana na uzembe wake katika Hospitali ambayo alipaswa kujua hapo awali alifanya makosa makubwa ya upasuaji” - amesema Mjane wa Marehemu.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!