Moshi wa kupikia Wasababisha vifo milioni 3.1 kwa mwaka 2021 pekee - UNEP

Moshi wa kupikia Wasababisha vifo milioni 3.1 kwa mwaka 2021 pekee - UNEP

Kwa mabilioni ya watu katika ulimwengu unaoendelea, hasa watoto na wanawake, muda wa chakula huanza kwa kuwasha jiko la mafuta ya taa, kuwasha jiko la mkaa au kuwasha moto magogo.

Tatizo: shughuli nyingi za kupika hufanyika ndani na moshi unaozalishwa umebeba chembe za sumu. Aina hii ya uchafuzi huu wa hewa unaofanyika majumbani ulisababisha vifo vya mapema vya watu milioni 3.1 mnamo 2021 na ni sehemu ya shida kubwa inayosababisha mabadiliko ya tabianchi na upotezaji wa bayonuai.

" Uchafuzi wa hewa nyumbani ni mojawapo ya matishio makubwa zaidi ya afya ya umma duniani na ni hatari kwa watoto," anasema Martina Otto, Mkuu wa Sekretarieti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira, (UNEP), "lakini habari njema ni kwamba teknolojia safi ya kupikia ni nyingi, si ghali, na tayari inasaidia kuokoa maisha. Changamoto iliyopo sasa ni kuweka teknolojia hii mikononi mwa watu wengi zaidi.”

Hata hivyo, uchafuzi wa hewa majumbani bado ni tatizo la afya na mazingira ambalo halijawekezwa sana duniani.

Tarehe 7 Septemba, Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi kwa ajili ya anga ya buluu huadhimishwa, ambayo imeundwa ili kuongeza ufahamu kuhusu hatari za uchafuzi wa hewa.

Hapa tuangazie sababu za uchafuzi wa hewa majumbani, na jinsi mbinu safi za kupikia zinaweza kuokoa maisha, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupambana na upoteaji wa viumbe hai.

Uchafuzi wa hewa majumbani umeenea kwa kiasi gani?

Ulimwenguni kote, karibu mtu mmoja kati ya watatu hupika kwenye majiko yasiyofaa au kwenye moto ulio wazi, akipumua moshi hatari kutoka kwa kinachojulikana kama nishati ngumu kama vile kuni, mkaa na kinyesi cha wanyama. Tatizo ni kubwa sana barani Afrika, ambapo takriban watu wanne kati ya watano wanakabiliwa na uchafuzi wa hewa nyumbani. Hiyo ni sehemu ya janga kubwa zaidi la uchafuzi wa hewa. Asilimia 99 ya watu duniani hupumua hewa ya majumbani au nje ambayo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linaiona si salama.

Uchafuzi wa hewa wa nyumbani ni nini hasa?

Kuna aina nyingi za uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba, ikiwa ni pamoja na uvundo, asbestosi na hewa ukaa. Lakini wakati wataalam wanarejelea uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba, wanazungumza hasa juu ya uchafu unaotokana na majiko yasiyofaa na mioto ya wazi. Miongoni mwa uharibifu zaidi kati ya hizi ni vipande vidogo mno vya uchafu, vumbi, moshi, masizi na kaboni nyeusi inayojulikana kama chembe ndogo.

Uchafuzi wa hewa wa nyumbani hufanya nini kwa mwili wa binadamu?

Chembe chembe ndogo chini ya saizi ya mikroni 10 - ambayo ni chini ya upana wa nywele za binadamu - inaweza kuingia kwenye mapafu na mkondo wa damu.

Kutoka huko, inaweza kusababisha matatizo makubwa ya afya, ikiwa ni pamoja na nimonia, ugonjwa wa moyo, kiharusi na kansa ya mapafu, uzito mdogo wa kuzaliwa na kuharibika kwa mimba.

Ni nani anayeteseka zaidi kutokana na uchafuzi wa hewa wa nyumbani?

Uchafuzi wa hewa majumbanii ni mbaya kwa kila mtu. ulisababisha vifo vya mapema vya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 3.1 mwaka 2021. Watoto wako hatarini zaidi kwa sababu wanapumua kwa kasi zaidi kuliko watu wazima - maana yake wanavuta hewa chafu zaidi - na mifumo yao ya kinga bado inaendelea kukua, na kuwaacha uwezo wao wa kupigana na ugonjwa. Mnamo mwaka 2021, uchafuzi wa hewa wa nyumbani ulisababisha vifo vya watoto 237,000 chini ya miaka mitano. Uchafuzi wa hewa ya nyumbani pia huathiri wanawake kwa njia isiyo sawa, kwani mara nyingi wanapika. Katika Afrika, wanawake na watoto ni asilimia 60 ya vifo vya mapema vinavyohusiana na kuvuta moshi na uchafuzi wa hewa wa nyumbani, kulingana na Shirika la Kimataifa la Nishati.

Nishati safi ya kupikia nini?

Ufafanuzi wa kawaida wa upikaji safi ni aina yoyote ya mafuta na jiko ambavo vinakidhi miongozo ya WHO kwa ubora wa hewa ya ndani ya nyumba. Hiyo kwa kawaida hujumuisha majiko yanayoendeshwa na umeme, gesi asilia, ethanoli na gesi ya kioevu ya petroli, ambayo ni safi na yenye ufanisi zaidi kuliko aina nyingine za mafuta magumu. Inaweza pia kujumuisha majiko yanayotumia mkaa wenye ufanisi wa juu ambao hutoa moshi mdogo kuliko majiko ya jadi ya majani.

Ulimwengu unawezaje kuongeza utumiaji nishati safi ya kupikia?

Uchafuzi wa hewa majumbani bado ni tatizo la afya na mazingira ambalo halijawekezwa zaidi duniani. Hiyo inahitaji kubadilika. Ulimwenguni, dola za Marekani bilioni 10 kwa mwaka zinahitajika kufikia mwaka 2030 ili kufikia upatikanaji wa upishi safi, kulingana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati (IEA).

Uwekezaji wa sasa ni sehemu tu ya hiyo. "Kwa kuzingatia maendeleo ya kiteknolojia na kupunguzwa kwa bei katika teknolojia ya kupikia inayotegemea jua, tunahitaji kuhakikisha kuwa kuna ufadhili wa bei nafuu kwa kaya kununua."

Martina Otto, Mkuu wa Sekretarieti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira, (UNEP), anasema. Pia anasisitiza umuhimu wa kuangazia malengo ya kupikia safi - hasa malengo ya kupikia kwa umeme.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!