Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,chanzo chake:
Kwa Mujibu wa shirika la Afya Duniani(WHO);
Mtoto huzaliwa na Uzito mdogo(Low birth weight) ikiwa amezaliwa na Uzito chini ya Grams 2500(< 2500 grams (5.5 pounds).
Je,Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,chanzo chake ni nini?
✓ Kutokana na "American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG)";
Kuna Sababu kubwa Mbili zinazopelekea mtoto kuzaliwa na tatizo la Uzito mdogo, na Sababu hizo ni;
- Mtoto kutokukua akiwa tumboni-Intrauterine growth restriction (IUGR)
- Pamoja na Mtoto kuzaliwa mapema/kabla ya wakati(preterm birth).
- Tatizo hili la mtoto kutokukua akiwa tumboni au mtoto kudumaa katika ukuaji wake tumboni(Fetal growth restriction/ intrauterine growth restriction) Hii ina maana mtoto haongezeki uzito anaopaswa kuongezeka kabla ya kuzaliwa.
Watoto wengine wanaweza kuzaliwa na uzito mdogo kwa sababu wazazi wao ni wadogo. Wengine wanaweza kuzaliwa na uzito mdogo kwa sababu kuna kitu kilipungua au kusimamisha ukuaji wao wakati wa ujauzito.
Kuna Umuhimu mkubwa wa mama mjamzito kufanya vipimo kama Ultrasound n.k ili kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni ikiwa ni pamoja na Ukuaji wake.
Vitu hivi huongeza hatari ya Mtoto kuzaliwa na Uzito Mdogo
1. Uchungu kuanza Mapema(Preterm labor).
Hii ina maana ya Uchungu ambao huanza mapema kabla ya wakati wake au kabla ya wiki 37 za Ujauzito,
Hali hii huweza kuongeza hatari ya mtoto kuzaliwa mapema kabla ya wakati wake na pia mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo la uzito mdogo.
2. Matatizo ya kudumu(Chronic health conditions).
Hizi ni hali za afya ambazo hudumu kwa muda mrefu au hutokea tena na tena kwa muda mrefu.
Matatizo haya ya kudumu ambayo huweza kuongeza hatari ya mtoto kuzaliwa na Uzito mdogo ni pamoja na;
- Tatizo la presha(high blood pressure),
- Tatizo la kisukari
- Matatizo ya Moyo
- Matatizo kwenye mapafu
- Pamoja na matatizo ya Figo
3. Matumizi ya baadhi ya Dawa
Baadhi ya dawa huweza kuongeza hatari ya kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo, mfano baadhi ya dawa za kutibu presha ya kupanda,tatizo la kifafa(epilepsy) au tatizo la blood clots.
Mwambie mtoa huduma wako kuhusu dawa yoyote unayotumia. Huenda ukahitaji kuacha kutumia dawa au kutumia dawa ambayo ni salama zaidi wakati wa ujauzito.
4. Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali
Baadhi ya maambukizi hasa yale yanayoathiri via vya uzazi vya Mwanamke kipindi cha Ujauzito huweza kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni,
baadhi ya maambukizi hayo ni pamoja na;
- cytomegalovirus,
- rubella,
- chickenpox,
- toxoplasmosis
- Na baadhi ya magonjwa ya Zinaa(certain sexually transmitted infections).
5. Matatizo kwenye kondo la nyuma au placenta.
Placenta hukua ndani ya uterasi na kumpatia mtoto chakula pamoja na oksijeni kupitia kwenye kitovu.
Baadhi ya Matatizo kwenye placenta yanaweza kupunguza mtiririko wa oksijeni na virutubisho kwa mtoto, hali ambayo inaweza kuathiri/kupunguza ukuaji wa mtoto.
6. Mama Kutoongezeka Uzito wa kutosha wakati wa Ujauzito
Wajawazito ambao hawaongezeki uzito wa kutosha wakati wa ujauzito wana uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kuliko wale wanaongezeka uzito kwa kiwango sahihi.
7. Mama mjamzito kuwa na tatizo la kushindwa kula(eating disorder)
Kama mama mjamzito hali vizuri basi hata mtoto aliyetumboni hawezi kupata virutubisho vya kutosha, hali ambayo huweza kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni na hata kupelekea kuzaa mtoto mwenye matatizo mbali mbali ikiwemo hili la uzito mdogo.
8. Kuwa na mimba ya mtoto zaidi ya mmoja
Tafiti zinaonyesha Zaidi ya nusu ya wakinamama ambao hubeba mimba ya watoto zaidi ya mmoja mfano;
Watoto wawili-mapacha(twins),watoto watatu(triplets) n.k) huwa za uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto wenye uzito mdogo.
9. Kuzaa watoto wenye Uzito mdogo kwenye ujauzito uliotangulia
Pia baadhi ya Tafiti zinaonyesha,wakina mama ambao wamewahi kuzaa watoto wenye uzito mdogo kwenye mimba za nyuma,wana uwezekano mkubwa wa kuzaa tena watoto wenye uzito mdogo.
10. Wanaokunywa Pombe na Wavutaji wa Sigara
Wajawazito wanaovuta sigara wana uwezekano zaidi ya mara 3 wa kupata mtoto ambaye ana uzito mdogo sana wakati wa kuzaliwa kuliko wale wasiovuta sigara,
Vivyo hivo matumizi ya Pombe wakati wa Ujauzito huongeza hatari zaidi ya Kujifungua watoto wenye tatizo la Uzito mdogo.
Kuvuta sigara, kunywa pombe, kutumia dawa za kulevyia, na kutumia vibaya dawa zilizoagizwa na daktari wakati wa ujauzito kunaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa mtoto tumboni na kuongeza hatari ya kuzaliwa kabla ya wakati pamoja na kuzaliwa na kasoro mbali mbali.
11. Vurugu na Vipigo nyumbani.
Hapo ndipo mwenzi wako anapokuumiza au anakudhulumu, Inajumuisha unyanyasaji wa kimwili, kingono na kihisia.
Vitu hivi huongeza hatari ya kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni,mimba kutoka,uchungu kuanza kabla ya wakati na kujifungua watoto kabla ya wakati, hali ambayo huongeza hatari ya kuzaa mtoto mwenye Uzito mdogo.
12.Umri wa kubeba Mimba na Kuzaa
Kubeba mimba Kwenye na Umri mdogo sana (hasa chini ya miaka 15) au kubeba mimba kwenye umri mkubwa zaidi ya miaka 35 hukufanya uwe na uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwenye uzito mdogo kuliko wazazi wengine.
Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,Pamoja na Vitu vinavyoongeza hatari zaidi ya kujifungua watoto wenye Uzito mdogo(Low-birthweight babies).
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!