Muda wa kumeza dawa pamoja na maelekezo yake

 MUDA WA KUMEZA DAWA PAMOJA NA MAELEKEZO YAKE

Kwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakitumia dawa pasipo kuzingatia matumizi sahihi ya muda kwenye Dawa husika.

Tatizo ambalo huweza kusababisha mtu kujioverdose Dawa bila yeye kujua.

Mfano: Utakutana na mtu anasema yeye kaambiwa ameze dawa asubuh na jion, au kutwa mara tatu, hivo anameza asubuh mchana na jion,

bila kujua asubuh na jion ni masaa mangapi au kutwa mara tatu ni masaa mangapi toka kumeza dawa.

NB: Kwa kuliona hilo, Leo nimeamua kukuandalia makala hii ambayo itakufungua macho, na kukusaidia kuzingatia muda sahihi kwenye matumizi ya dawa ulizopewa.

Pia itakusaidia wewe kuepuka kujioverdose dawa,badala yake utatumia dawa kwenye kiwango sahihi pamoja na muda sahihi unaotakiwa.

MUDA WA KUMEZA DAWA PAMOJA NA MAELEKEZO YAKE

1. Ukiambiwa dawa hizi meza kutwa MARA TATU au kwa kitaalam unaweza andikiwa kwa kifupi "tds"

- Maana yake unatakiwa kumeza dawa hizi KILA BAADA YA MASAA 8.

hivo kutwa mara tatu sio asubuh, mchana na jion tu, no ila ni kila baada ya masaa 8.

2. Ukiambiwa dawa hizi meza kutwa MARA MBILI, Haina maana ya asubuh na jion tu

- Bali,maana yake unatakiwa kumeza dawa hizi KILA BAADA YA MASAA 12.

3. Ukiambiwa dawa hizi meza kutwa MARA MOJA, au kwa kitaalam unaweza andikiwa kwa kifupi "OD" Ikiwa na maana ya ONCE PER DAY.

- Maana yake unatakiwa kumeza dawa hizi KILA BAADA YA MASAA 24.

mfano: kama umemeza dawa leo saa moja kamili asubuh ni mpaka kesho saa moja kamili asubuhi(hayo ndyo masaa 24).

Nimatumaini yangu kwamba umeelewa matumizi sahihi ya MUDA kwenye dawa ulizopewa.

KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!