NDOA ZA UTOTONI NA MADHARA YAKE
Kama nilivyokwisha kuelezea kwenye utangulizi wangu ndani ya baadhi ya makala zinazohusu Mimba za utotoni,
Mojawapo ya matokeo ya Ndoa za utotoni ni Mimba za utotoni,
Bado katika jamii zetu vitendo hivi vipo,watoto wanaolewa wakiwa wadogo kabsa na kupata mimba wakiwa watoto.
MADHARA YA NDOA ZA UTOTONI
-Moja ya hasara kubwa ambayo wengi wao wanapata ni kukatishwa masomo yao na kushindwa kuzifikia Ndoto zao
- Kuanza majukumu makubwa ya kutunza Familia ukiwa bado mtoto
- Kuendelea kuwa na hali mbaya kiuchumi
- Kuendelea kuwa na hali mbaya ya kiafya
- Kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa mbali mbali ya Zinaa katika umri mdogo kama vile;kaswende,kisonono,pangusa(chlamydia) n.k
- Kuwa kwenye hatari ya kupata Maambukizi ya virusi vya UKIMWI
- Kuwa kwenye hatari ya kupatwa na Saratani ya mlango wa kizazi yaani Cervical Cancer
- Kubeba Mimba kwenye umri mdogo na kupata madhara makubwa kama vile;
• Kujifungua kwa upasuaji
• Kuchanika Njia ya kujifungulia
• Kuchanika tumbo la uzazi
• Kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua
• Kupatwa na magonjwa kama Fistula n.k
• Kupoteza maisha n.k
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!