Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Ruto atangaza maombolezo ya siku tatu kufuatia Moto Shuleni ulioua 18



Rais Ruto atangaza maombolezo ya siku tatu kufuatia Moto Shuleni ulioua 18

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu baada ya watoto 18 kufa kwa kuungua moto kwenye bweni, katika shule ya msingi ya Hillside Endarasha katika kaunti ya Nyeri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio makamu wa Rais Rigathi Gachagua, alisema wanafunzi 70 hawajulikani walipo na 27 wako hospitali.

Gachagua ameutaja mkasa huo kuwa wa kutisha na kusema kwamba kazi ya uchunguzi kwa kutumia vinasaba DNA itahitajika ili kusaidia kuwabaini wahanga na kutoa wito kwa jamii kusaidia katika kuwatafuta waliopotea.

Polisi wa Kenya wameimarisha uchunguzi wao baada ya kutokea mkasa huo wa moto. Msemaji wa polisi ya Kenya Resila Onyango, ameliambia shirika la Habari la AFP kwamba miili iliyopatikana katika eneo la tukio ilikuwa imeteketezwa kiasi cha kutoweza kutambuliwa. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Taharuki imetanda miongoni mwa wanafamilia wa watoto huku wakiwa wamekusanyika shuleni hapo wakisubiri kupata taarifa juu ya wapendwa wao ambao hawajapatikana bado.

Kulingana na jeshi la polisi, miili ya watoto iliyopatikana katika eneo la ajali imeungua kiasi cha kutotambulika.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasaidiana na mashirika mengi ya kukabiliana na hali ya dharura na pia linatoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi na wanafamilia waliopata kiwewe.

Muchai Kihara, mwenye umri wa miaka 56, amesema amebahatika kumpata mwanawe Stephen Gachingi mwenye umri wa miaka 12 akiwa hai alipokimbilia shuleni hapo mwendo wa saa saba mchana siku ya Ijumaa.

Amesema ana furaha kubwa kwa kuwa mwanawe yuko hai ingawa alipata majeraha sehemu ya nyuma ya kichwa chake na macho yake yameathiriwa na moshi.

Katikati mwenye tai nyekundu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya akiwa katika shule ya illside Endarasha Academy, katika mji wa Kieni, kaunti ya Nyeri.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Kenya imekumbwa na mikasa ya moto katika miaka ya nyuma, mnamo mwaka 2016, wanafunzi tisa walikufa baaya ya kuungua moto katika shule ya sekondari ya wasichana katika mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi.

Mnamo mwaka 2001, wanafunzi 67 waliuawa katika shambulio la kuchomwa moto bweni lao katika shule ya upili katika mji wa Machakos ulio kusini mwa jiji la Nairobi.

Wanafunzi wawili walishtakiwa kwa mauaji, na mwalimu mkuu na naibu wake walipatikana na hatia ya kuwa wazembe.

Nchi Jirani za Tanzania na Uganda pia zimekumbwa na mikasa ya shule kuchomwa moto iliyosababisha hasara.

Chanzo: AFP



Post a Comment

0 Comments