Ticker

6/recent/ticker-posts

Sababu ya harufu mbaya kwapani,Soma hapa kufahamu



Sababu ya harufu mbaya kwapani,Soma hapa kufahamu

• • • • •

TATIZO LA KUNUKA KIKWAPA(chanzo na tiba)

Tatizo la kunuka kikwapa huweza kuwa kero kubwa kwa watu, japo kuna wengine hawafahamu kwamba huu unaweza kuwa ugonjwa kabsa wala sio kwa sababu mtu hajaoga.

Zipo sababu ambazo huweza kusababisha kikwapa chako kutoa harufu ikiwa ni pamoja na swala la usafi, ila katika makala hii nazungumzia tatizo la kunuka kikwapa kama ugonjwa.

CHANZO CHA TATIZO LA KUNUKA KIKWAPA

Shida hii huweza kutokana na maambukizi ya vimelea mbali bali vya magonjwa kama vile Fangasi pamoja na Bacteria.

Hali ya maji maji,jasho na unyevu unyevu kwapani huvutia na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya vimelea hivi kushambulia eneo hili.

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

- Mtu kuwashwa maeneo ya kwapani

- Kwapa kuwa na ukavu sana pamoja na kutoa unga unga

- Kwapa kutoa maji maji yasio yakawaida

- Kwapa kuvuja jasho kupita kawaida

- Kwapa kutoa harufu mbaya sana

N.k

JINSI YA KUJIKINGA NA KUTIBU TATIZO HILI

✓ Fanya usafi wa maeneo ya kwapani kila mara ikiwa ni pamoja na kuoga mwili mzima

✓ Vaa nguo safi,epuka kuvaa nguo chafu kama vile: shati,tishet N.k

✓ Tumia dawa mbali mbali za fangasi pamoja na bacteria

✓ Punguza matumizi ya vyakula ambavyo vina viungo vingi

✓ Epuka kuogea sabuni ambazo zina kiasi kikubwa cha kemikali

N.k

KUMBUKA; unaweza kukutana na wataalam wa afya ukaongea nao na kupata tiba sahihi kwa ajili ya tatizo lako

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments