Sababu ya kichwa kuuma asubuhi baada ya kuamka

Sababu ya kichwa kuuma asubuhi baada ya kuamka

Baadhi ya watu hupatwa na tatizo la maumivu ya kichwa wakati wa asubuh mara tu baada ya kuamka kutoka usingizini, je ni nini chanzo chake?

HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA TATIZO HILI

- Kuwa na tatizo la kupata shida ya Kupumua wakati umelala

- Tatizo la Kukoroma, Sio watu wote wanaokoroma wanapata shida ya kupumua wakati wa kulala,

Hata hivyo, kukoroma peke yake kunaweza kuwa sababu ya maumivu ya kichwa wakati wa asubuhi.

Katika utafiti mmoja uliohusisha watu 268 wanaokoroma mara kwa mara, asilimia 23.5% waliamka wakiwa na maumivu ya kichwa asubuhi mara kwa mara.

- Mtu Kukosa Usingizi au kutokulala vizuri usiku

- Kulala kupita kiasi, Kulala kupita kiasi kunaweza pia kusababisha maumivu ya kichwa asubuhi.

- Tatizo la Kusaga Meno wakati umelala kwa kitaalam Sleep bruxism,

tatizo hili la kusaga meno wakati wa kulala, linaweza kukufanya uamke na maumivu ya kichwa.

- Kuwa na Hangover, Kunywa sana Pombe jioni kunahusishwa sana na maumivu ya kichwa asubuhi.

Hata hivyo, hata katika viwango vya chini, pombe huathiri usingizi na inaweza kusababisha maumivu ya kichwa asubuhi.

- Matatizo kama Circadian Rhythm Disorders

Watu walio na matatizo kama haya wanapata maumivu ya kichwa asubuhi mara nyingi zaidi kuliko wale wasio na tatizo hili.

- Matumizi ya Baadhi ya Dawa n.k

ZINGATIA MAMBO HAYA KAMA UNATATIZO HILI

• Weka Ratiba yako ya Kulala vizuri: Unashauriwa kuLala na uamke kwa wakati mmoja kila siku.

• Fanya Mazoezi Mara kwa Mara: Jaribu kufanya mazoezi angalau saa kadhaa kabla ya kulala

KUMBUKA: Kufanya mazoezi karibu sana na wakati wako wa kulala kunaweza kukufanya uwe macho kwa muda mrefu.

• Punguza Kafeini na Pombe, kunywa Kahawa alasiri au glasi ya pombe kabla tu ya kulala inaweza kukufanya uchelewe kulala au kutatiza usingizi wako.

• Rekebisha Mazingira Yako ya Kulala: Unahitaji nafasi na mazingira ya giza, mazingira tulivu na yasio na kelele kabsa.

• Pata muda wa Mapumziko, epuka kufanya kazi kupita kiasi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!