Ticker

6/recent/ticker-posts

Shida Ya Ganzi Miguuni(Miguu Kufa Ganzi)



 SHIDA YA GANZI MIGUUNI(MIGUU KUFA GANZI)

Watu wengi wamekuwa wakichanganya ganzi na hisia nyingine kama miguu kuwaka moto, kutekenywa na hata kuhisi kukanyaga kitu chenye ncha kali.

Kufa ganzi ni kitendo cha kupoteza hisia katika sehemu husika. Tatizo/ kitendo hiki kinaweza kuwa ni cha muda mfupi au muda mrefu na kinaweza kuwa baadhi ya sehemu au sehemu mbalimbali.

Hali hii inaweza kuwa ni dalili ya shida katika mfumo wa fahamu.

Mtu anapogusa kitu hisia au taarifa hupokelewa na vipokeo vilivyo katika ngozi kisha husafirishwa na mishipa ya neva mpaka kwenye uti wa mgongo na kisha kwenye ubongo kwaajili ya kutafasiriwa. Na baada ya ubongo kuchakata taarifa hizi hurudisha taarifa kupitia mishipa ya neva mpaka eneo husika.

Kufa ganzi hupelekea kupoteza uwezo wa kuhisi kuguswa, joto, kuhisi maumivu na mitetemo na baadhi ya watu hupelekea kushindwa kutambua zilipo sehemu husika za mwili wao.

Kufa ganzi hupelekea kukosekana kwa hisia/taarifa na kunaweza pelekea mtu kupata maambukizi, vidonda na majeraha yanayoweza kupelekea majanga ya kukatwa mguu au sehemu husika.

SABABU ZA MIGUU KUFA GANZI

Kufa ganzi hutokea iwapo kuna changamoto katika njia ya usafirishaji wa hisia/ taarifa. Shida hii inaweza tokeo kwenye vipokeo(receptors), mishipa ya neva, uti wa mgongo au ubongo.

Miongoni mwa mambo yanayoweza haribu njia hii ya usafirishwaji wa taarifa/hisia ni

1. Kupungua au kuzuiwa kwa usafirishwaji wa damu kwenda kwenye mishipa ya neva mfano kwenye kiharusi (stroke)

2. Ajari au magonjwa ambayo yanashambulia mishipa ya neva

3. Kukandamizwa kwa neva (mfano watu wenye tatizo za pingili za mgongo, uvimbe, usaha au mabonge ya damu yatokanayo na ajari)

4. Upungufu wa vitamin hasa vitamin B12

5. Sumu, madawa na kemikali kali

6. Magonjwa kama kisukari na magonjwa ya figo

7. Magonjwa yatokanayo na kinga mwili kushambulia mishipa ya neva.

DALILI AMBAZO HUWEZA KUAMBATANA NA KUFA GANZI.

Chanzo/sababu ya kufa ganzi inaweza kugundulika kutokana na dalili ambazo zimeambatana kwamfano

1. Maumivu ya mgongo na shingo, kichwa na viungo

2. Homa na mabakamabaka mwilini kwa baadhi ya wagonjwa

3. Miguu kukakamaa sana hasa pale unapohitaji kutembea

4. Kushindwa kunyoosha miguu au mguu n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments