Ticker

6/recent/ticker-posts

Tahadhari wanaotumia ARVs kunenepesha mifugo



Tahadhari wanaotumia ARVs kunenepesha mifugo 

Serikali na Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba Tanzania (TMDA) zimetoa tahadhari ya matumizi  ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs) kunenepesha mifugo, ikitajwa kuwa ni athari kwa afya ya jamii.

Mbali na usugu unaosababishwa na ARV, utafiti uliofanyika mwaka 2018 ulionyesha kuwa asilimia 90 ya wafugaji wanatumia dawa za antibiotiki kutibu wanyama badala ya chanjo.

TMDA imetoa onyo hilo Jana Jumapili, Septemba 22, 2024 ikiwa ni siku mbili tangu wanasayansi, watafiti kukutana kujadili, matumizi holela ya ARV yanavyochangia usugu wa dawa hizo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo imeeleza kuwa mamlaka imepata taarifa juu ya uwepo wa baadhi ya wafugaji wanaotumia vibaya dawa hizo kwa lengo la kunenepesha mifugo yao, akikemea matumizi hayo kwa kuwa yana madhara kwa afya ya jamii.

Kwa upande wake,  Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria za nchi na suala hilo linaanza kufuatiliwa na Wizara ya Afya na Wizara ya Mifugo na uvuvi kwa pamoja.

“Serikali haikubaliani na hili, yeyote anayefanya hivyo anakiuka kanuni na taratibu, kwa hiyo TMDA wanafuatilia ili kujua nani anafanya na hatua za kisheria zitafuata kwa watakaobainika,” amesema Msasi.

Via;Mwananchi



Post a Comment

0 Comments