Tatizo la Bacterial vaginosis,chanzo,dalili na Tiba yake

 Tatizo la Bacterial vaginosis,chanzo,dalili na Tiba yake

Bacterial Vaginosis ni tatizo linalohusisha maambukizi ya bacteria ukeni, na kwa asilimia kubwa hutokana na kuongezeka kwa bakteria wa kawaida kwenye uke(overgrowth) ambao huvuruga usawa wa asili Ukeni au kukosekana kwa uwiano kati ya bacteria wabaya na wale bacteria wazuri waliopo ukeni.

Japo tatizo hili huweza kumpata Mwanamke wa Umri wowote ila Wanawake ambao wapo kwenye umri wa uzazi(reproductive age) huwa kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO HILI LA BACTERIAL VAGINOSIS NI PAMOJA NA;

- Mwanamke kutokwa na uchafu ukeni ambao ni Mwepesi, wenye rangi nyeupe, kijivu au Kijani

- Kutokwa na Uchafu ukeni wenye harufu mbaya kama shombo ya Samaki(Foul-smelling "fishy" vaginal odor)

- Kupatwa na Miwasho sehemu za siri au Ukeni(Vaginal itching)

- Mwanamke kuhisi hali ya kuungua Wakati wa kukojoa n.k

Pia Wanawake wengi wanaweza kuwa na tatizo hili la bacterial vaginosis bila kuonyesha dalili zozote.

UKIPATA DALILI HIZI KAFANYE VIPIMO

• Kutokwa na uchafu ukeni ambao ni Mwepesi, wenye rangi nyeupe, kijivu au Kijani

• Kutokwa na Uchafu ukeni wenye harufu mbaya kama shombo ya Samaki(Foul-smelling "fishy" vaginal odor)

• Kuanza kupata Homa n.k

CHANZO CHA TATIZO LA BACTERIAL VAGINOSIS

Bacterial Vaginosis ni tatizo linalohusisha maambukizi ya bacteria ukeni, na kwa asilimia kubwa hutokana na kuongezeka kwa bakteria wa kawaida kwenye uke(overgrowth) ambao huvuruga usawa wa asili Ukeni au kukosekana kwa uwiano kati ya bacteria wabaya na wale bacteria wazuri waliopo ukeni.

Bacteria wazuri "good" bacteria (lactobacilli) na bacteria wabaya"bad" bacteria (anaerobes). Hawa bacteria wabaya "anaerobic bacteria" wakiwa wengi zaidi hubadilisha kabsa mazingira asilia ya ukeni kisha kupelekea tatizo la bacterial vaginosis.

VITU HIVI HUONGEZA HATARI ZAIDI YA MWANAMKE KUPATA TATIZO HILI LA BACTERIAL VAGINOSIS;

1. Kuwa na Wapenzi wengi(Multiple sexual partners)

2. Kufanya ngono zembe, mapenzi bila kinga/Condom

3.Kufanya douching mara kwa mara, kutumia sabuni zenye kemikali zaidi ukeni,kupaka mafuta yenye kemikali ukeni, spray,kuingiza vitu kama toys au vidole mara kwa mara ukeni n.k

4. Kuwa na upungufu wa bacteria wazuri(good bacteria) yaani lactobacilli bacteria ukeni, hii huweza kuongeza hatari ya kupata bacterial vaginosis.

MADHARA YA TATIZO LA BACTERIAL VAGINOSIS

- Huweza kupelekea kujifungua mtoto kabla ya wakati yaani Preterm birth.

- Kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa mengine ya zinaa ikiwemo Kisonono(gonorrhea), chlamydia,herpes simplex virus, pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

- Kuongeza hatari ya kidonda cha mama aliyefanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi(hysterectomy) kushambuliwa na bacteria yaani post-surgical infection.

- Kuwa kwenye hatari ya kupata tatizo la maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke yaani Pelvic inflammatory disease (PID).

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA

- Medical history taking

- Pelvic Examination, ikiwemo njia ya kutumia vidole viwili kuingiza ukeni na kupima, Ultrasound n.k

- Kuchukua Sample ya Uchafu unaotoka ukeni na kwenda kuupima( taking Vaginal Secretions)

- Vaginal PH Test

MATIBABU YA TATIZO HILI LA BACTERIAL VAGINOSIS

Baadhi ya dawa ambazo huweza kutumika kutibu tatizo hili

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!