Tatizo la korodani ya mtoto mchanga kupanda juu kuelekea tumboni
Tatizo la korodani ya mtoto mchanga kupanda juu kuelekea tumboni
Tatizo hili huhusisha Korodani za mtoto kutokushuka chini ndani ya Kifuko chake cha ngozi ambayo inaning'inia chini ya Uume(scrotum) na hutokea kabla hata ya mtoto hajazaliwa,
Mara nyingi tatizo hili huhusisha Korodani Moja, Lakini pia shida hii huweza kutokea kwa Korodani zote Mbili.
Pia shida hii huweza kutokea zaidi kwa watoto ambao huzaliwa kabla ya wakati,yaani watoto njiti au Premature,
Tatizo hili ni rahisi Kugundulika, wakati Mtoto anafanyiwa uchunguzi(newborn examination) mara tu baada ya kuzaliwa,
Ni muhimu sana kwa mzazi,kama umeona mabadiliko yoyote kwa sehemu za Siri za mtoto wako,uliza kwanza au ongea na watalam wa afya ili wamchunguze mara moja mtoto wako.
CHANZO CHA TATIZO HILI KWA WATOTO
Chanzo halisi cha tatizo hili bado hakijulikani,ila Sababu hizi hapa chini zimeonekana kuwa na uhusiano wa karibu sana na kuongeza hatari ya mtoto kuzaliwa na tatizo hili;
- Matumizi ya Pombe Kwa Mama wakati wa UJAUZITO
- Mtoto kuzaliwa na tatizo la Uzito Mdogo
- Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati,Mtoto Njiti(Premature)
- Kuwa na Historia ya tatizo hili kwenye Familia yako
- Uvutaji wa Sigara kwa Mama Wakati wa Ujauzito, au Kukaa karibu na Mtu ambaye anavuta Sigara mara kwa mara wakati wa Ujauzito
- Mama Mjamzito kukaa kwenye mazingira yoyote yenye kemikali au Sumu, kama vile za dawa yaani pesticides n.k
- Matatizo yoyote ambayo huweza kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni kama vile; tatizo la Down syndrome n.k
MADHARA YA TATIZO HILI NI YAPI?
Lengo Kubwa la korodani kuning'inia kwa Nje ni ili kubalance Joto, na kutengeneza mazingira mazuri ya afya ya Uzazi kwa Ujumla,ikiwemo,swala la utengenezaji wa mbegu za kiume n.k
Hii ni kwasababu Ili korodani zikue,zikomae na kufanya kazi vizuri,zinahitaji joto ambalo kidogo Lipo chini ukilinganisha na Joto la Mwili yaani Body temperature,
Na mazingira hayo yapo kwenye eneo hili la Scrotum Peke yake.
Sasa je,Ni madhara yapi endapo Korodani za Mtoto hazijashuka kama kawaida? SOMA HAPA ZAIDI..!!!
1. Saratani ya Korodani, Tafiti zinaonyesha Wanaume ambao Korodani zao hazijashuka kama kawaida wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Saratani yaani Testicular cancer.
Saratani kwenye Korodani huanza kwenye Seli ndani ya Korodani ambazo zimeshindwa kuzalisha mbegu za kiume zilizokomaa,
Japo kinachobadilisha hizi seli kuwa Saratani bado hakifahamiki.
2. Matatizo ya Uzazi, Mtoto wako atakapokua Mkubwa anaweza kuwa kwenye hatari ya kupatwa na matatizo mbali mbali ya uzazi kama vile;
- Kuwa na tatizo la kuzalisha kiwango kidogo cha Mbegu za kiume yaani Low Sperm counts
- Kuzalisha mbegu za Kiume zenye ubora wa chini sana
- Na vyote hivi hupelekea shida ya Mwanaume kushindwa kumpa MIMBA mwanamke.
3. Kupatwa na tatizo la Testicular,ambapo mrija wa mbegu za kiume(spermatic cord) ambao ndani yake una vimishipa vidogo vya Damu,Nerves pamoja na tube ya kusafirisha mbegu za kiume huweza kubanwa,kujikunja n.k
Hii huweza kupelekea maumivu sehemu za korodani.
4. Korodani zenyewe kuumia,kutokana na kutokuwa Sehemu sahihi, Kisha kuathiriwa na mgangamizo au Pressure kwenye eneo hili.
5. Kupatwa na tatizo la Hernia yaani Inguinal hernia n.k.
MATIBABU YA TATIZO HILI
Wakati mwingine Korodani za mtoto hushuka na kurudi mahali pake zenyewe,Ila Endapo Korodani za mtoto hazijashuka mpaka atakapofikisha umri wa kuanzia miezi 4, Basi Korodani hizi haziwezi kurudi zenyewe tena.
Mtoto akipata Tiba Mapema,basi hupunguza zaidi kupatwa na madhara ambayo nimeyataja hapo juu,
Hasa akitibiwa kabla ya kufikisha Umri wa Mwaka Mmoja,
• Matibabu ni Pamoja na UPASUAJI, ambapo inashauriwa Mtoto kufanyiwa Upasuaji kabla ya kufikisha Umri wa miezi 18.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!