Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo La Kuvimba Pua Wakati Wa Ujauzito(Stuffy Nose) Chanzo Na Tiba Yake



TATIZO LA KUVIMBA PUA WAKATI WA UJAUZITO(STUFFY NOSE) CHANZO NA TIBA YAKE

Tatizo la kuvimba pua sio la kushangaa kwani hutokea kwa baadhi ya wanawake na sio kitu cha ajabu, tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Stuffy Nose,ambapo Mwanamke huvimba pua wakati akiwa mjamzito.

CHANZO CHA TATIZO LA KUVIMBA PUA WAKATI WA UJAUZITO

1. Mwili kuzalisha maji mengi zaidi yaani extra fluid hali ambayo hupelekea mama mjamzito kuvimba kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wake kama vile; kuvimba Miguuni,mikononi,usoni,kwenye Pua n.k

2. Mishipa ya damu kutanuka zaidi ili kupitisha damu nyingi zaidi kutokana na mahitaji kuongezeka,Ikiwa damu inahitajika kwa mama na mtoto pia,

hali hii ya kutanuka au kuvimba kwa mishipa ya damu puani husababisha ujazo wa damu kuongeza(Blood volume) na mama mjamzito kupatwa na shida ya kuvimba pua

3. Mabadiliko ya vichocheo mwilini kipindi cha ujauzito, mfano;

- Kuongezeka kwa kichocheo(hormone) cha Oestrogen kipindi cha ujauzito huongeza mtiririko wa damu yaani Blood flow kuelekea kwenye Mucous membrane ambazo zipo kwenye pua, hali hii huweza kusababisha Pua kuvimba

- Hormone za ukuaji yaani Growth hormone kutoka kwenye kondo la nyuma au Placenta, huweza kuhusishwa pia na shida ya Pua kuvimba wakati wa ujauzito,

Uvimbe(tumor) ambao huweza kukua kwenye tezi linalojulikana kama Pituitary gland ambalo linazalisha Growth hormones huweza kusababisha shida ya Nasal Congestion au pua kuvimba n.k

4. Tatizo la kuwa na msukumo mkubwa wa damu kipindi cha ujauzito yaani High blood pressure huweza pia kuongeza uwezekano wa mama mjamzito kupatwa na shida hii ya pua kuvimba

KUMBUKA; Mabadiliko yote ambayo hutokea kipindi cha ujauzito huisha yenyewe na mwili kurudi kwenye hali yake ya kawaida kabsa ndani ya kipindi cha wiki 6-7(siku 42) baada ya mama kujifungua.

MAMBO YAKUZINGATIA KAMA UNA TATIZO LA KUVIMBA PUA WAKATI WA UJAUZITO NI PAMOJA NA;

- Punguza matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula chako wakati wa ujauzito

- Hakikisha unakunywa maji ya kutosha angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku, hii tu sio itakusaidia kwenye shida hii,pia na kwenye matatizo mengine kama vile kupunguza uwezekano wa kupatwa na UTI za mara kwa mara n.k

- Hakikisha unadhibiti presha yako, na kama una dalili ambazo huzielewi ongea na wataalam wa afya kwa msaada zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments