Connect with us

afyatips

Tatizo la kuweweseka, kuona vitu visivyo na uhalisia (hallucinations)

Doctor Ombeni

Published

on

Tatizo la kuweweseka, kuona vitu visivyo na uhalisia (hallucinations)

Unaweza kupata shida ya kuweweseka usiku na kuona vitu visivyo na uhalisia tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama hallucinations.

Hallucinations ni pale unaposikia, kuona, kunusa, kuonja au kuhisi vitu vinavyoonekana kuwa halisi lakini vipo tu akilini mwako,Kwa hali ya kawaida Vitu hivi watu wengine hawavioni.

Pata usaidizi wa kimatibabu ikiwa wewe au mtu mwingine ana tatizo hili la Hallucinations.

Aina za Hallucinations

Unaweza kuwa na hallucinations kama:

  1. Unasikia Sauti ambazo hakuna mtu mwingine anayesikia
  2. Kuona vitu,watu,taa,hisia ya kuguswa,vitu kutembea mwilini mwako n.k ambavyo si halisi,
  3. kuhisi harufu ya vitu ambavyo havipo, kuwa na ladha ya vitu ambavyo unahisi tu havipendezi au ni vya ajabu
  4. Kuhisi Mwili wako unaruka,kupaa n.k wakati sio kweli.

Chanzo cha tatizo la kuweweseka na kuona vitu visivyo halisi(Hallucinations)

Hallucinations inaweza kusababishwa na hali nyingi tofauti za kiafya zinazoathiri hisia,

Sababu zinazochangia tatizo la hallucinations kwa kiasi kikubwa ni pamoja na:

– Hali ya afya ya akili ikiwemo uwepo wa matatizo kama vile ;

  • schizophrenia
  • au bipolar disorder

– Matumizi ya dawa za kulevyia

– Matumizi ya Pombe

– Magonjwa kama vile;

  • Alzheimer’s disease
  • Au Parkinson’s disease

– Kuwa na matatizo ambayo huathiri hali ya uono wa macho,  Kusababisha mabadiliko au kupoteza uwezo wa macho kuona vizuri,

Matatizo kama vile;Charles Bonnet syndrome n.k

– Kuwa na tatizo la wasiwasi sana, huzuni au msiba/kufiwa

– Athari kutokana na matumizi ya baadhi ya dawa(side effects)

– Baada ya upasuaji, dawa za usingizi(anesthesia) n.k

Wakati mwingine hallucinations inaweza kuwa ya muda mfupi. Inaweza kutokea ikiwa una tatizo la kuumwa kipandauso(migraines), joto la mwili kuwa juu sana au tu unapoamka au kulala.

Pia hallucinations inaweza kusababishwa na maambukizi, uvimbe kwenye ubongo au tatizo la kuchanganyikiwa (delirium), hasa kwa watu wazee.

Ni rai yangu kwako kama unatatizo la kuweweseka na kuona vitu visivyo na uhalisia, hakikisha unapata msaada haraka.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti23 hours ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...