Tatizo la Leukopenia,Chanzo,dalili na Tiba Yake
Leukopenia ni tatizo linalohusisha kushuka kwa Idadi ya Seli nyeupe Za Damu(low white blood cell count).
Seli nyeupe za Damu(white blood cells-WBCs) ni sehemu muhimu kwenye mfumo wako wa kinga ya mwili. Zinasaidia mwili wako kupigana na magonjwa au maambukizi mbali mbali. Ikiwa una Seli nyeupe za damu(WBCs) chache sana, una hali inayojulikana kama leukopenia.
Aina mbali mbali za tatizo la leukopenia
Kuna aina kadhaa tofauti za leukopenia, kulingana na aina gani ya seli nyeupe(WBCs) iliyo chini katika damu yako,
Aina za Seli nyeupe za damu(WBCs) ni pamoja na:
- neutrophils
- lymphocytes
- monocytes
- eosinophils
- basophils
Jedwali hapa chini linaonyesha viwango vya kawaida vya Seli Nyeupe za damu(WBCs), kulingana na Leukemia and Lymphoma Society.
WBCs (per μL of blood) | |
Men | 5,000 to 10,000 |
Women | 4,500 to 11,000 |
Children | 5,000 to 10,000 |
Dalili za tatizo la leukopenia?
Unaweza usione ishara au dalili zozote za tatizo la leukopenia, Lakini kama idadi ya seli nyeupe za damu ziko chini sana, unaweza kuwa na dalili zikiwemo:
1. Kupata homa, au joto kuwa juu kwa 100.4˚F (38˚C) au Zaidi
2. Mwili kutetemeka
3. Kutoa Jasho sana mwilini
4. Kuwa na shida ya sore throat
5. Kupata shida ya kukohoa
6. Kuanza kuishiwa na Pumzi
7. Au kupata dalili zingine za maambukizi kama vile;
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa
- Kupata vidonda mdomoni
- Kuwa na sehemu ya mwili wako ambayo imekuwa nyekundu, kuvimba, au kuwa na maumivu n.k
Chanzo cha tatizo la leukopenia
Magonjwa pamoja na hali nyingi zinaweza kusababisha tatizo la leukopenia, kama vile:
- Kuwa na tatizo kwenye Seli za damu au kwenye Uboho(Blood cells or bone marrow conditions)
Seli nyeupe za damu(WBCs) hutoka kwenye seli shina yaani stem cells kwenye uboho. Kwa sababu ya hili, hali zinazoathiri seli za damu au uboho zinaweza kusababisha tatizo la leukopenia. Baadhi ya mifano ya hali kama hizi ni pamoja na:
- Tatizo la aplastic anemia
- leukemia
- lymphoma
- multiple myeloma
- myelodysplastic syndrome
- myeloproliferative syndrome
- myelofibrosis
- Kuwa na tatizo kwenye bandama, Wengu au bandama ni muhimu katika utengenezaji wa Seli nyeupe za damu(WBCs). tatizo la kuvimba kwa bandama au kwa kitaalam "Splenomegaly", huweza pia kusababisha tatizo la leukopenia.
- Matibabu ya Saratani, Matibabu ya saratani yanalenga kuondoa seli za saratani zinazogawanyika haraka ndani ya mwili wako,
Walakini, kwa sababu seli za damu pia hukua haraka, matibabu mengine ya saratani yanaweza kuharibu seli hizi pia. Matibabu ya saratani ambayo yanaweza kusababisha tatizo la leukopenia ni pamoja na:
- chemotherapy
- Pamoja na radiation therapy (hasa inapotumika kwenye mifupa mikubwa, kama ile ya miguu na mfupa wa nyonga)
- Upandikizaji wa uboho(bone marrow transplants)
- Matatizo ambayo unazaliwa nayo (Congenital disorders)
Matatizo wakati wa kuzaliwa yanayoweza kusababisha tatizo la leukopenia ni pamoja na yale yanayoathiri jinsi uboho unavyofanya kazi kutengeneza seli za damu, kama vile:
- Tatizo la Kostmann syndrome, au severe congenital neutropenia
- myelokathexis n.k
- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali au tunasema magonjwa ya kuambukiza yaani Infectious diseases
Baadhi ya Magonjwa ya kuambukiza ambayo huweza kusababisha tatizo la leukopenia ni pamoja na;
- Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV or AIDS)
- Ugonjwa wa TB(tuberculosis)
- viral hepatitis
- malaria
Au magonjwa mengine kama vile Homa ya matumbo(typhoid fever),
Maambukizi mengine ya virusi ya papo hapo, kama vile Flu(mafua), au maambukizi yoyote makali sana yanaweza pia kusababisha tatizo la leukopenia.
- Matatizo kwenye mfumo wa kinga mwili(Autoimmune disorders)
Baadhi ya matatizo ya kingamwili yanaweza kuua Seli nyeupe za damu(WBCs) au seli za shina za uboho, ambazo hutengeneza seli za damu, na kupelekea kusababisha tatizo la leukopenia,
Mifano ya matatizo kwenye kinga mwili ambayo yanaweza kusababisha tatizo la leukopenia ni:
- lupus
- rheumatoid arthritis
- Sjögren’s syndrome
- Tatizo la Utapiamlo(Malnutrition), Pia tatizo la Leukopenia huweza kusababishwa na upungufu wa baadhi ya Virutubisho muhimu mwilini kama vile;vitamins au madini, Mfano; upungufu wa;
- vitamin B12
- folate
- copper
- zinc n.k
- Matumizi ya baadhi ya dawa, Pia baadhi ya dawa huweza kuchangia uwepo wa tatizo la leukopenia kama side effects,
Mfano ni dawa kama vile;
- bupropion (Wellbutrin)
- carbimazole
- clozapine (Clozaril)
- cyclosporine (Sandimmune)
- interferons
- lamotrigine (Lamictal)
- minocycline (Minocin)
- mycophenolate mofetil (CellCept)
- penicillin
- sirolimus (Rapamune)
- tacrolimus (Prograf)
- valproic acid (Depakote)
- Tatizo la Sarcoidosis,
Sarcoidosis ni ugonjwa wa kimfumo unaosababishwa na mwitikio wa kinga uliokithiri. Unajulikana kwa kuundwa kwa granulomas, au maeneo madogo ya kuvimba katika mifumo mingi ndani ya mwili wako.
Wakati granulomas hizi zinaundwa kwenye uboho wako, hapa ndipo tatizo la leukopenia linaweza kutokea.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!