Tatizo la mdomo kukauka chanzo chake na Tiba yake

 Tatizo la mdomo kukauka chanzo chake na Tiba yake

Je unasumbuliwa na tatizo la kukauka mdomo pamoja na Lips zake?

Tatizo la Kukauka Mdomo kwa kitaalam hujulikana kama xerostomia na hutokea pale ambapo Tezi za mate (Salivary glands) hushindwa kutengeneza mate ya kutosha mdomoni hali ambayo hupelekea kushindwa kutengeneza mazingira ya unyevu unyevu mdomoni,

Na hii hutokea kwa Sababu mbali mbali ikiwemo;

- Matumizi ya baadhi ya Dawa, baadhi ya dawa zina side effect ya kukausha mdomo,

mfano; baadhi ya dawa za kutibu tatizo la depression,Wasiwasi(anxiety),Presha(high blood pressure), baadhi ya dawa za maumivu, dawa kwenye kundi la antihistamines,decongestants,pamoja na muscle relaxants.

- Umri kuwa Mkubwa(Aging), tafiti zinaonyesha watu wengi kadri umri unavyokuwa mkubwa zaidi ndivo hupata shida hii ya mdomo kukauka,

Na hili huenda sambamba na matumizi ya baadhi ya dawa,Mabadiliko kwenye mwili hasa kwa upande wa uwezo wa mwili kuchakata dawa, Lishe Duni pamoja na kuwa na matatizo mengine ya kiafya ya muda mrefu.

- Kukosa Virutubisho muhimu mwilini kama vile madini pamoja na Vitamins, mfano vitamin B,A N.k

Hii hutokana na Lishe duni, au kukosa Mlo wenye virutubisho vyote kwa kiwango sahihi kinachohitajika mwilini yaani balance diet.

- Matibabu ya Kansa au Saratani(Cancer therapy),

Mfano;Dawa za Chemotherapy huweza kubadilisha asili ya mate na kiasi kinachozalishwa.

Japo hali hii sio ya kudumu ni ya muda mfupi tu, mara baada ya mgonjwa kumaliza tiba, Uzalishwaji wa kawaida kwa mate hurudi tena kama awali.

Huduma ya Mionzi(Radiation treatments), hasa ikifanyika eneo la kichwani na shingoni, hii huweza kusababisha uharibifu wa tezi za Mate hali ambayo hupelekea kupungua sana kwa uzalishwaji wa Mate,

Hii nayo huweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kutegemea na radiation dose pamoja na eneo lililokuwa linatibiwa.

- Uharibifu wa Neva, hii huweza kutokea baada ya mtu kuumia(Injury) au kufanyiwa Upasuaji ambao husababisha uharibu wa nerves eneo la Kichwani na Shingoni,

Hii huweza kupelekea mtu kupata tatizo la mdomo kukauka.

- Matatizo mengine ambayo huweza kuchangia tatizo la Mdomo kukauka ni pamoja na;

• Ugonjwa wa Kisukari(Diabetes)

• Tatizo la kiharusi(Stroke)

• Maambukizi ya fangasi wa Mdomoni-yeast infection (thrush)

• Alzheimer's disease

• Au magonjwa yanayohusisha mfumo wa kinga mwili(autoimmune diseases), kama vile Sjogren's syndrome

• Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV/AIDS).

• Tatizo la Kukoroma na kupumua mdomo wako ukiwa wazi pia huweza kuchangia kinywa kuwa kikavu zaidi. n.k

- Matumizi ya tumbaku na Pombe. Uvutaji wa Sigara,kutumia tumbaku pamoja na Pombe, vyote hivi huweza kuchangia zaidi tatizo la mdomo kuwa mkavu

- Matumizi ya dawa za kulevyia,Mirungi(Marijuana) n.k

- Matumizi ya Recreational drugs kama vile Methamphetamine huweza kusababisha hali ya mdomo kukauka sana na kuharibu meno, tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama "meth mouth."

MADHARA YA TATIZO LA MDOMO KUKAUKA;

Kama huzalishi mate ya kutosha na mdomo wako ukakauka,hii inaweza kusababisha;

1. Meno yako kuwa kwenye hatari zaidi ya kuharibika(tooth decay)

2. Kupata magonjwa ya fizi yaani gum Diseases

3. Kupata vidonda mdomoni(Mouth sores)

4. Kuwa kwenye hatari zaidi ya kushambuliwa na fangasi wa mdomoni(Yeast infection)

5. kuwa na vidonda au ngozi kupasuka kwenye kona za mdomo

6. Lips za mdomo kupasuka(cracked lips)

7. Mdomo kutoa harufu mbaya n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!