Tatizo la meno kuvunjika(tatizo la meno kuwa na ukakasi)

 TATIZO LA MENO KUVUNJIKA(TATIZO LA MENO KUWA NA UKAKASI)

Tatizo hili la meno kuvunjika huweza kusababishwa na sababu zaidi ya moja na wakati mwingine huambatana na tatizo lingine la baadhi ya meno yako kuwa na ukakasi.

shida hii huweza kuhusisha jino moja, au meno zaidi ya moja,meno ya juu kwa mbele,meno ya nyuma n.k, kulingana na chanzo chake,

CHANZO CHA TATIZO LA MENO KUVUNJIKA.

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia meno kuvunjika kama vile;

- Umri, Shida ya meno kuvunjika yenyewe huweza kuwapata watu wenye umri mkubwa kuanzia Miaka 50 na kuendelea

- Meno huweza kuvunjika kutokana na mtu kula vyakula vigumu sana au kutafuna vitu vigumu sana,

unashauriwa kuepuka kutafuna vitu vigumu sana ikiwemo ile tabia ya kufungua visoda vya Bia au Soda kwa kutumia meno yako, hii huweza kusababisha meno kuvunjika,kupasuka,kutengeneza cracks au kutengeneza Kovu.

- Tabia ya kutafuna Barafu mara kwa mara(Ice chewing)

- Shida ya kusaga meno mara kwa mara yaani Teeth grinding (bruxism),

Tatizo hili huhusisha mtu kusaga meno bila yeye kupanga(Involuntary) hasa nyakati za usiku akiwa amelala.

- Watu wenye shida ya meno kutoboka(dental cavities) wapo kwenye hatari ya kupatwa na tatizo la meno kuvunjika na kutoka pia

- Huduma ya kuziba meno kwa kiwango kikubwa yaani kwa kitaalam Large dental fillings or a root canal, huweza kudhoofisha meno yako na hata kusababisha meno kuvunjika au kutoka.

- Kuumia kwa kudondoka chini,wakati wa michezo mbali mbali,wakati unaendesha pikipiki,baskeli,ajali ya gari au hata kupigana(ngumi),hii huweza kusababisha meno kuvunjika.

DALILI ZA TATIZO HILI LA MENO KUVUNJIKA NI PAMOJA NA;

• Mtu kupata maumivu kwenye sehemu ya jino hasa wakati wa kutafuna kitu chochote

• Mtu kuhisi hali ya tofauti sana mdomoni hasa wakati wa baridi au akila vitu vya baridi na vyakula vitamu(sweet foods).

• Sehemu inayozunguka Jino kuvimba

• Mtu kuonekana kwa Nje akiwa ameachama au kuongea n.k

MADHARA AMBAYO HUWEZA KUTOKEA BAADA YA JINO AU MENO KUVUNJIKA

✓ Sehemu ambapo jino limevunjika au kutengeneza Cracks huweza kushambuliwa na vimelea vya magonjwa kama bacteria na kusababisha matatizo kama tooth abscess n.k

✓ Mtu kupatwa na tatizo lingine la kutoa harufu mbaya mdomoni

✓ Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na Homa

✓ Maumivu ya jino au meno ambayo hayaishi

✓ Kupatwa na tatizo la Kuvimba kwa Fizi

✓ Kuvimba kwa tezi za Lymph nodes n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!