Tatizo La Mirija Ya Uzazi Kujaa Maji

 TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

Hydrosalpinx,hili ni tatizo la kujaa maji kwenye mirija ya uzazi au kwenye sehemu ya mwisho ya mirija ya uzazi na kisha kuvimba.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NI PAMOJA NA;

- Mwanamke kuwa na historia ya kupatwa na maambukizi kwenye via vyake vya uzazi mara kwa mara yaani pelvic inflammatory disease(PID)

- Mwanamke kuwa na historia ya kuumwa na kidole tumbo yaani Appendix kisha ikapasukia ndani

- Mwanamke kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa(Sexual transmitted diseases-STD's) kama vile; Ugonjwa wa kisonono(gonorrhea),tatizo la chlamydia n.k

- Tatizo la Endometriosis,ambapo huhusisha kukua kwa kuta za ndani ya tumbo la uzazi kuelekea nje

- Mwanamke kuwa na historia ya kufanyiwa upasuaji tumboni

- Mwanamke kupatwa na tatizo la maji kujaa kwenye mirija ya uzazi kisha kusababisha mirija ya uzazi kuziba na kuvimba,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hydrosalpinx

- Mwanamke kuwa na historia ya kupatwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi yaani Ectopic pregnancy

- Mwanamke kuwa na tatizo la uvimbe kwenye mirija ya uzazi yaani Fibroids n.k

DALILI ZA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

Kwa asilimia kubwa wanawake wengi wenye tatizo hili la kuziba mirija ya uzazi na mirija kujaa maji hawaonyeshi dalili zozote,mpaka pale watakapoanza kupata shida ya kutokubeba mimba,ndipo huamua kufanya vipimo na kugundulika shida hii, Lakini endapo watapata dalili,basi miongoni mwa dalili hizi hapa chini huweza kuonekana;

• Mwanamke kupata maumivu makali ya tumbo eneo la kwenye kitovu,chini ya kitovu,pembeni upande mmoja au kwenye kiuno

• Mwanamke kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi

• Mwanamke kupata maumivu ya tumbo upande mmoja,hii hutokea sana kwa wanawake ambao tatizo la mirija ya uzazi kuziba chanzo chake ni maji kujaa na kuziba kwenye mirija ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hdyrosalpinx

• Baadhi ya wanawake hupata shida ya kutoa damu ukeni yaani vaginal bleeding n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

✓ Kwanza ifahamike kwamba, mwanamke huweza kupata shida ya mirija ya uzazi kuziba upande mmoja au mirija yote miwili yaani kulia na kushoto,

Endapo kuziba kumetokea upande mmoja uwezekano wa mwanamke huyu kubeba mimba bado upo, ila Mwanamke huyu yupo pia kwenye hatari ya mimba hii kutunga nje ya kizazi, yaani kupatwa na tatizo la Ectopic pregnancy

Na endapo mirija yote miwili ya Uzazi imeziba ningumu sana kwa mwanamke huyu kubeba mimba mpaka atibiwe,

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA

Moja ya vipimo ambavyo huweza kufanyika ni pamoja na;

1. Kipimo cha Hysterosalpingograph(HSG),Kipimo hiki ni aina ya X-ray ambayo husaidia kuona ndani ya mirija ya uzazi

2. Na kipimo kingine ni Laparoscopy N.k

3. Kipimo cha Ultrasound n.k

MATIBABU YA TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

Moja ya tiba kwenye tatizo hili ni pamoja na Mwanamke kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe,kuondoa Scars, au huduma ya Kuzibua mirija,matumizi ya dawa mbali mbali n.k Kutegemea na chanzo cha tatizo lenyewe.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!