Tatizo la Mkazo wa macho(Eyestrain),chanzo,dalili na Tiba yake
Eyestrain ni tatizo la Mkazo wa macho ambalo husababishwa na Kutumia macho kwa muda mrefu wakati wa kutazama kitu flani, kama vile kutazama simu, skrini za kompyuta, kusoma vitabu, kuendesha gari au kutazama TV kwa muda mrefu.
Tunapoangalia kitu kilichopo karibu sana, kama vile skrini ya kompyuta au simu ya mkononi, lenzi ya jicho husinyaa kwa kawaida. Ikiwa unatazama skrini kwa muda mrefu, lenzi haina nafasi ya kupumzika, ambayo inaweza kusababisha uchovu wa macho,
Uchovu huu wa macho pia unatokana na kupungua kwa muda wa kufumba macho, Bila kupepesa macho wakati wa kutazama kwa muda mrefu, huweza kusababisha uoni hafifu na kuendelea kwa tatizo hili la mkazo wa macho(Eyestrain).
Dalili za tatizo la Mkazo wa macho(Eyestrain)
Dalili za Tatizo la Mkazo wa macho(Eyestrain) ni Pamoja na;
1. Macho kuwa mekundu, kutoa machozi na kuwasha
2. Kuhisi macho kuchoka kutazama au macho kuwa mazito hata kunyanyua, kope nzito n.k
3. Kuona Marue rue na kuwa na tatizo la kushindwa kutazama kitu kimoja kwa muda
4. Kupata maumivu ya kichwa kwa mbali(Mild headache).
5. Kupata tatizo la misuli kukakamaa eneo la macho au kwenye kope(Muscle spasms)
6. Kutokuwa na uwezo wa kuendelea kufungua macho
Kumbuka; Dalili za tatizo la mkazo wa macho(Eyestrain) zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya macho, kwa hivyo ni bora kuongea na daktari wako wa macho kwa utambuzi.
Nini cha kufanya endapo una tatizo hili la Mkazo wa macho(Eyestrain)?
Dalili za tatizo la mkazo wa macho(eyestrain) mara nyingi hupunguzwa kwa kufanya haya;
✓ Kupumzisha macho,
Hivo epuka kutazama vitu kama Simu,computer,TV, au kusoma Vitabu kwa muda mrefu
✓ Kubadilisha mazingira ya kazi ili kupunguza Mwanga kuakisi, kung'aa na mwanga mkali
✓ Kuvaa miwani sahihi kulingana na tatizo lako n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!