TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA SIKU ZAKE ZA HEDHI
Tatizo hili la Mwanamke kukosa siku zake za hedhi kwa kitaalam hujulikana kama Amenorrhea,
ambapo huweza kutokea mara moja au zaidi, kwenye Kukosa hedhi kuna Vitu viwili; tuna Primary na Secondary amenorrhea
(1) Primary amenorrhea,Hii inahusu kutokuwepo kwa hedhi kwa Mwanamke ambaye hajapata hedhi kufikia umri wa miaka 15.
Sababu za kawaida za aina hii ya kukosa hedhi ni pamoja na viwango vya homoni, ingawa matatizo ya Kimaumbile pia yanaweza kusababisha shida hii.
(2) Secondary Amenorrhea,Hii inahusu Mwanamke kukosa hedhi ndani ya vipindi vitatu au zaidi mfululizo kwa mwanamke ambaye amekuwa akipata hedhi hapo awali.
Mimba ndio sababu ya kawaida ya kukosa hedhi hii kwenye secondary amenorrhea, ingawa matatizo ya homoni pia yanaweza kusababisha shida hii.
[sc_fs_faq html="true" headline="h3" img="" question="Amenorrhea ni Tatizo gani?" img_alt="" css_class=""] Tatizo hili la Mwanamke kukosa siku zake za hedhi kwa kitaalam hujulikana kama Amenorrhea, [/sc_fs_faq]
KUMBUKA,Kwa Upande wa Tiba,Matibabu ya tatizo la Kukosa hedhi yanategemea na chanzo husika.
Moja ya vitu ambavyo wanawake wengi hupata shida sana ni pale ambapo hawaoni siku zao za hedhi,
katika makala hii tumechambua baadhi ya sababu ambazo huweza kusababisha Mwanamke kutokupata siku zake za hedhi(Miss period).
BAADHI YA SABABU HIZO NI KAMA VILE;
1. Ujauzito, Hii ndyo sababu kubwa ambayo husababisha Wanawake Wengi kutokuona siku zao za hedhi,
ndyo maana wanawake wengi wasipoona siku zao za hedhi,kitu cha kwanza ambacho wanawaza ni MIMBA.
2. Tatizo la Stress, Wanawake wengi hawajui ukiwa na msongo wa mawazo au STRESS, inaweza kuvuruga kabsa mzunguko wako wa hedhi,
Stress huweza kusababisha Mwanamke kublid kwa muda mrefu, kuzidisha maumivu wakati wa hedhi,kublid kwa muda mfupi sana kuliko kawaida, au kutokuona kabsa siku zake za hedhi.
3. Kupungua uzito wa mwili kwa gafla(Sudden weight loss), Fahamu kwamba kupungua uzito wa mwili kwa kiasi kikubwa sana au kwa gafla huweza kusababisha Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi,
Hii ni kwasababu ya kuzuiwa kwa uzalishwaji wa hormones au vichocheo ambavyo huhitajika kwa ajili ya kitendo cha Ovulation.
4. Kuwa na uzito mkubwa kuliko inavyotakiwa(overweight/obesity), ukiwa na shida hii ya uzito mkubwa huweza kusababisha mwili wako kuzalisha kiwango kikubwa sana cha vichocheo vya OESTROGEN,
Uzalishwaji mwingi wa Hormone hii huweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi ikiwemo na kuchangia Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi.
5. Mwanamke kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi, ukiwa unafanya mazoezi kwa kiasi kikubwa sana huweza kuathiri hormones zinazohusika na kurekebisha mzunguko wako wa hedhi ikiwa ni pamoja na kukosa siku za hedhi hasa pale ambapo mwili hupoteza kiasi kikubwa cha mafuta(body fat) wakati wa mazoezi.
6. Matumizi ya njia mbali mbali za uzazi wa mpango, Wanawake wengi wanaotumia njia za uzazi wa mpango kama vile vidonge, vijiti,Sindano n.k huweza kukosa siku zao za hedhi kama ilivyokawaida.
Ingawa siku zako za hedhi hutakiwa kurudi kwenye hali yake yakawaida baada ya kuacha kutumia njia hizi.
7. Mwanamke kufikia kipindi cha ukomo wa hedhi yaani Menopause, Mwanamke anapokaribia ukomo wa hedhi,huanza kutokuona siku zake za hedhi,
Hii ni kwasababu kiwango cha Oestrogen huanza kupungua sana na mzunguko wa hedhi huanza kutokueleweka kabsa, kitendo cha Ovulation hakifanyiki tena Na hapa ndipo hufata hali hii ya mwanake kukosa kabsa siku zake za hedhi,
8. Sababu zingine ni matatizo kama vile; Tatizo la Polycystic ovary syndrome (PCOS), na wakati mwingine matatizo kama
• Magonjwa ya moyo
• Kuwa na ugonjwa wa kisukari ambao haujadhibitiwa(uncontrolled diabetes)
• Shida ya Overactive thyroid n.k
DALILI ZA AMENORRHEA
Dalili Za Tatizo hili la Kukosa Hedhi(Amenorrhea)
Kulingana na sababu ya amenorrhea, unaweza kupata ishara au dalili zingine pamoja na kutokuwepo kwa hedhi, kama vile:
• Kutokwa na maziwa kwenye chuchu
• Kupoteza nywele
• Kupata Maumivu ya kichwa
• Mabadiliko kwenye kuona
• Kuwa na Nywele nyingi usoni
• Kupata Maumivu ya nyonga
• Kuwa na Chunusi n.k
MADHARA YA TATIZO HILI LA KUKOSA HEDHI,
Je kuna madhara yoyote ya kukosa hedhi, Ndyo kulingana na chanzo cha kukosa Hedhi
Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababisha matatizo mengine pia,Ikiwa ni pamoja na:
1. Mwanamke kushindwa kubeba Mimba,
Ikiwa hupati ovulation na hupati hedhi, huwezi kuwa mjamzito,
Wakati mwingine tatizo la kukosa hedhi hutokana na shida kwenye vichocheo mwilini,Kutokuwa na Usawa wa vichocheo mwilini(hormones imbalance),
Hii huweza kusababisha hata Usibebe Ujauzito
2. Pia inaweza kusababisha kuharibika kwa mimba au matatizo mengine wakati wa ujauzito.
3. Matatizo ya kisaikolojia, Mwanamke kukosa hedhi wakati wenzako wanapata huweza kusababisha hali ya mfadhaiko,msongo wa mawazo n.k, haswa kwa vijana ambao wanabadilika kuwa watu wazima.
4.Kupatwa na matatizo mengine kama vile Osteoporosis na ugonjwa wa moyo(cardiovascular disease),
Matatizo haya mawili yanaweza kusababishwa na kutokuwa na kiwango cha estrogen ya kutosha.
Osteoporosis ni tatizo linalohusisha kudhoofika kwa mifupa,
cardiovascular disease ni ugonjwa wa moyo ambao huweza kuleta shida kwenye mishipa ya damu na misuli ya moyo.
5. Kupata Maumivu ya nyonga. Ikiwa tatizo la Kimaumbile linasababisha amenorrhea,
Hii inaweza pia kusababisha maumivu katika eneo la nyonga(Pelvic).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!