Ticker

6/recent/ticker-posts

TMA yafafanua Mvua zinazoendelea kunyesha nchini



TMA yafafanua Mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema, mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mengi nchini Tanzania hivi sasa ni za nje ya msimu ambazo zinasababishwa na upepo unaotoka baharini.

Imesema, mvua za msimu wa vuli bado hazijaanza na zitaanza mwanzoni mwa Oktoba hadi Desemba huku zikitarajiwa kuwa za wastani na chini ya wastani nchini.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Septemba 5, 2024,  Meneja Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema, mvua zinazonyesha kwa sasa ni za nje ya msimu ambazo zinapita.

"Zinasababishwa na upepo unaotoka Mashariki ambao tunao mpaka sasa unaotoka baharini kuja kwenye maeneo yetu.

"Upepo huo unachukua unyevunyevu ambao upo baharini hivyo kusababisha hizi mvua zinazoendelea ambazo hazimaanishi msimu umeanza," amesema.

Amesema, msimu wa vuli utaanza mwanzoni mwa Oktoba ingawa amebainisha utakuwa na mvua za kusuasua na za mtawanyiko usioridhishia kutokana na uwepo wa hali ya La-Nina katika eneo la kati la Kitropiki la Bahari ya Pasifiki.

#mwananchiupdates



Post a Comment

0 Comments