Ugonjwa wa chalazion,chanzo,dalili na Tiba
chalazion ni tatizo la kuwa na kauvimbe kwenye eneo la kope yako(Tazama mfano kwenye Picha hapo)
Wakati mwingine tatizo hili la Chalazion huitwa eyelid cyst au meibomian cyst,
Shida hii Inatokea polepole wakati tezi ya mafuta inayoitwa meibomian inapozibwa.
Kwa baadhi ya Watu Chalazion inapotokea kwa Mara ya kwanza, inaweza kuhusisha maumivu lakini baada ya muda kidogo hupati maumivu yoyote.
Chalazion kawaida hutokea kwenye kope za juu lakini mara nyingine pia inaweza kutokea kwenye kope za chini.
CHANZO CHA TATIZO LA CHALAZION
Chalazion inaweza kutokea wakati tezi ndogo ya mafuta kwenye kope ikiziba au kuzuiwa na kitu chochote,
Tezi hizi husaidia sana kwenye kufanya macho yawe na unyevu unyevu,
Tezi iliyoziba au kuzuiwa na kitu chochote huanza kubakiza mafuta na kuvimba,
Hatimaye kupelekea kutokea kwa uvimbe mgumu kwenye kope yako.
-Baadhi ya sababu Zingine za ziada zinazopelekea kutokea kwa chalazion ni pamoja na;
- Tatizo la Rosacea (hali ya ngozi ambayo husababisha wekundu na chunusi kwenye ngozi).
- Chronic blepharitis,
- Tatizo la kuvimba kwa kope yaani eyelid inflammation
- Tatizo la Seborrheic dermatitis
- Tatizo la Tuberculosis (TB).
- Maambukizi ya virusi(Viral infections).n.k
DALILI ZA CHALAZION
Dalili za chalazion ni nini?
Unapokuwa na tatizo la chalazion, utaona dalili zifuatazo:
- Kutokewa na kauvimbe pasipo maumivu yoyote kwenye kope yako,Na mara nyingi hutokea kwenye eneo la juu ya Kope
- Kuwashwa kidogo, na kusababisha macho kutoa machozi kwa baadhi ya watu
- Kupata shida ya Kuona vizuri hasa chalazion ikiwa Kubwa zaidi
CHALAZION HUGUNDULIWAJE?
Kwa kawaida unashauriwa kuonana na mtaalamu wa macho unapokuwa na chalazion,
Unaweza kuonana na daktari wa macho au ophthalmologist. Watoa huduma hawa wa afya wanaweza kuchunguza chalazion na kutoa maelekezo sahihi kuhusu matibabu.
Unapomwona mtaalamu wa macho, unapaswa kutarajia haya;
- Kujua Historia ya Ugonjwa wako,
Toa historia yako kamili ya tatizo lako lilivyoanza, Maelezo haya yanaweza kumsaidia mtoa huduma wako kupata vitu vya kuanza navyo kwa haraka zaidi,
- Uchunguzi wa nje wa macho: Mtoa huduma wako atachunguza jicho lako, kope Pamoja na umbile la ngozi,
- Uchunguzi wa kina wa kope: Wataalamu wa macho huweza kutumia vifaa maalum kwa ajili ya uchunguzi zaidi machoni
MATIBABU YA TATIZO HILI
Zipo njia mbali mbali kwa ajili ya matibabu ya Tatizo hili,
Pamoja na vitu vya kufanya na kuzingatia Ukiwa Nyumbani na ukakaa Sawa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!