Ugonjwa wa eczema,Ukurutu au Pumu ya Ngozi,chanzo chake,Dalili na Tiba

 Ugonjwa wa eczema,Ukurutu au Pumu ya Ngozi,chanzo chake,Dalili na Tiba

Eczema ni ugonjwa wa ngozi ambao huhusisha hali ya mabaka mabaka ya ngozi,ngozi kuwaka moto, kuwasha, kupasuka n.k. Aina zingine za Eczema zinaweza pia kusababisha malengelenge.

Tatizo hili la Eczema hujulikana kama Ugonjwa wa Ukurutu au Pumu ya Ngozi,

Watu wengi hutumia neno ukurutu(eczema) wanapohusisha Atopic dermatitis ambayo ndiyo aina inayojulikana zaidi. Aina hii ya atopic dermatitis huhusisha zaidi mfumo wa kinga ya mwili, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa ngozi au kuvimba kwa ngozi, pumu na Homa za mara kwa mara.

Vyakula vingine, kama vile karanga na maziwa, vinaweza kusababisha dalili zaidi za eczema pamoja na Vichochezi vya mazingira kama moshi, baadhi ya sabuni, baadhi ya mafuta ya kupaka na kupikia,manukato n.k

DALILI ZA UGONJWA HUU WA ECZEMA(UKURUTU AU PUMU YA NGOZI)

Dalili za ugonjwa Huu zinaweza kutofautiana kulingana na umri wa mtu, ukali wa hali hiyo na zinaweza kutofautiana kwa mtu na mtu.

(1). Dalili za jumla za eczema ni pamoja na:

- Ngozi kuwa kavu sana na magamba

- Mtu kupata shida ya ngozi kuwasha

- Kuhisi hali ya kuungua sana kwenye ngozi

- Ngozi kuwa nyekundu kwenye baadhi ya maeneo

- Ngozi kubadilika na kuwa na mabaka mabaka yanayowasha, na wakati mwingine kuwa na upele,malenge lenge au vidonda. N.K

(2). Dalili za Eczema kwa watoto wachanga

Dalili zifuatazo za ugonjwa huu wa ngozi ni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 2:

- vipele juu ya kichwa na mashavu

- vipele vinavyotoka kabla ya kuvuja maji

- upele ambao unaweza kusababisha Muwasho sana, na kusababisha mtoto kushindwa kulala

(3). Dalili za eczema kwa watoto wa Miaka 2 na Zaidi.

Dalili zifuatazo za ugonjwa huu wa ngozi ni kwa watoto wenye umri wa miaka 2 na zaidi:

- upele unaoonekana nyuma ya mikunjo ya viwiko au magoti

- vipele vinavyoonekana kwenye shingo, viganja vya mkono, vifundoni na mpasuko kati ya matako na miguu.

- vipele vya matuta

- vipele vinavyoweza kuwa vidogo vidogo sana na vyeusi zaidi

- Ngozi kuvimba au kuwa nene zaidi kwa kitaalam hujulikana kama lichenification, na kuwa na muwasho wa kudumu,

Watoto wengi walio na hali hii huipata kabla ya umri wa miaka 5.

(4). Dalili za Eczema kwa watu wazima

Dalili zifuatazo za ugonjwa huu wa ngozi hutokea kwa watu wazima:

- vipele ambavyo vina magamba zaidi kuliko vinavyotokea kwa watoto

- vipele ambavyo kwa kawaida huonekana kwenye mikunjo ya viwiko au magoti au sehemu ya shingo.

- vipele vinavyofunika sehemu kubwa ya mwili

- ngozi kuwa kavu sana kwenye maeneo yaliyoathirika

- vipele ambavyo huwashwa sana n.k

CHANZO CHA UGONJWA HUU WA NGOZI NI NINI?

Ugonjwa huu wa eczema(Ukurutu au Pumu ya ngozi) huweza kuhusishwa na sababu mbali mbali ikiwemo;

• Sababu za Kigenetics, ambapo vinasaba vya tatizo hili huweza kutokea kwenye familia,

Watu ambao wana ndugu wenye shida hii ya Eczema, wenye Asthma au seasonal allergies wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu wa ngozi.

• Tatizo la kiutendaji kwenye mfumo wako wa kinga ya Mwili

• Pia baadhi ya tafiti zinaonyesha tatizo hili huweza kutokea kwa wakina mama ambao wanapata watoto kwenye umri mkubwa sana kuliko wale ambao wanajifungua mapema

• Sababu za kimazingira,ikiwemo uchafuzi wa mazingira,kukaa sehemu zenye kemikali za sumu zaidi,n.k

• Matatizo mengine ya ngozi ambayo huweza kuhusisha ngozi kuwa na jeraha,na kuruhusu maji maji kutoka nje pamoja na vimelea vya magonjwa kupenya ndani

• Matatizo kama Endocrine disorders ikiwemo thyroid disease n.k

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA NGOZI

Kwa sasa hakuna tiba ya eczema,Matibabu huhusisha zaidi kudhibiti dalili za ugonjwa huu ikiwemo ngozi iliyoathirika.

(1)Mambo ambayo unaweza kufanya ukiwa nyumbani;

Kuna mambo kadhaa ambayo watu wenye eczema wanaweza kufanya ili kusaidia afya ya ngozi na kupunguza dalili.

Mambo hayo ni kama vile;

- kuoga kwa maji ya uvuguvugu

- kupaka moisturizer ndani ya dakika 3 baada ya kuoga

- Kuhakikisha ngozi haiwi kavu kila siku kwa kupaka mafuta n.k

- Kuvaa nguo za pamba pamoja na vitambaa laini, na kuepuka nguo za kubana sana na zenye nyuzi mbaya ambayo huweza kuleta mikwaruzo.

- Kuepuka matumizi ya sabuni zenye kemikali zaidi,mafuta ya kupaka au manukato ya aina yoyote.

- kuweka kucha fupi ili kuzuia mikwaruzo kwenye ngozi.

Watu wanaweza pia kujaribu tiba mbalimbali za asili za ukurutu, ikiwa ni pamoja na aloe vera, mafuta ya nazi n.k

DAWA;

Zipo dawa kadhaa ambazo huweza kutumika kudhibiti dalili za eczema kama vile:

✓ Dawa za kupaka(Topical corticosteroid creams and ointments):

✓ Dawa za vidonge vya kunywa(Oral medications): Jamii ya corticosteroids au immunosuppresants.

✓ Dawa jamii ya Antibiotics,Antihistamines: n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!