UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU(DEMENTIA),chanzo,dalili na tiba
Ugonjwa wa dementia ni ugonjwa unaohusisha kuharibika kwa seli hai za ubongo kutokana na mjumuisho wa magonjwa mengi ambayo husababisha mtu kupoteza uwezo wa kumbu kumbu kichwani,uwezo wa kufikiria,uwezo wa kutatua matatizo, uwezo wa kuongea N.K
Na miongoni mwa magonjwa makubwa ambayo husababisha Shida hii ya Dementia ni pamoja na Ugonjwa wa Alzheimer's, ugonjwa huu huchangia kwa wastani wa asilimia ya 60% mpaka 80%.
Sababu zingine ambazo huchangia kutokea kwa tatizo hili la Dementia ni pamoja na;
- Mtu kuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu (severe depression)
- Unywaji wa pombe kupita kiasi
- Madhara yatokanayo na matumizi ya baadhi ya dawa
- Upungufu au ukosefu wa vitamins Mwilini
- Matatizo yatokanayo na tezi aina ya Thyroid
DALILI ZA UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU NI PAMOJA NA;
- Mtu kupoteza uwezo wake wa kutunza kumbu kumbu kichwani
- Mtu kuwa na shida katika kuongea lugha yake
- Mtu kuwa na shida katika kufanya maamuzi yake
- Uwezo wa mtu katika kufikiria mambo huathirika kwa kiwango kikubwa
MATIBABU YA UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU(DEMENTIA)
• Hakuna matibabu ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Dementia, ila kuna tiba juu ya kuthibithi dalili mbali mbali zinazojitokeza kwa Mgonjwa wa Dementia.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!